Posted By Posted On

MORRISON APEWA NDINGA MPYA NA BOSI SIMBA, ATUMA UJUMBE WA KIJEMBE KIMTINDO

  BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba ameonyesha furaha yake na kushukuru kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’ kwa kuonyesha picha ya gari ambayo inatajwa kuwa amepewa zawadi na bosi huyo ndani ya Simba.Morrison amejiunga na Simba akitokea Klabu ya Yanga ambapo dili lake la usajili lilileta utata kwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake wa zamani Yanga ambao walieleza kuwa nyota huyo ana mkataba wa miaka miwili huku yeye akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita.Sakata hilo ambalo lilivuta hisia za mashabiki na wadau wa mpira lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 makau makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi kutokana na makosa yaliyogundulika kwenye mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tarehe ndani ya mkataba wake.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ameonyesha picha mpya ya gari  na kuandika maneno ya shukrani kwa bosi wa Simba ‘Mo’ huku akiweka ujumbe wa utani kama kijembe kwa wale ambao wanaeleza kuwa hajali wachezaji.”Asante sana Mo, ni mfano wa kiongozi mkubwa, asante Simba ni hatua nyingine,endeleeni kusema kwamba hajali wachezaji wake.”,

  


BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba ameonyesha furaha yake na kushukuru kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’ kwa kuonyesha picha ya gari ambayo inatajwa kuwa amepewa zawadi na bosi huyo ndani ya Simba.


Morrison amejiunga na Simba akitokea Klabu ya Yanga ambapo dili lake la usajili lilileta utata kwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake wa zamani Yanga ambao walieleza kuwa nyota huyo ana mkataba wa miaka miwili huku yeye akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita.

Sakata hilo ambalo lilivuta hisia za mashabiki na wadau wa mpira lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 makau makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi kutokana na makosa yaliyogundulika kwenye mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tarehe ndani ya mkataba wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ameonyesha picha mpya ya gari  na kuandika maneno ya shukrani kwa bosi wa Simba ‘Mo’ huku akiweka ujumbe wa utani kama kijembe kwa wale ambao wanaeleza kuwa hajali wachezaji.

“Asante sana Mo, ni mfano wa kiongozi mkubwa, asante Simba ni hatua nyingine,endeleeni kusema kwamba hajali wachezaji wake.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *