Posted By Posted On

NYOTA MPYA WA RUVU SHOOTING, DACOSTA AANZA NA MAJANGA

 NYOTA mpya ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting yenye maskani yake Pwani, Adam Dacosta ameanza na majanga baada ya kuumia kidole.Dacosta aliibukia ndani ya Ruvu Shooting akitokea Klabu ya Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.Akizungumza na Saleh Jembe, Dacosta amesema kuwa ameshindwa kucheza mechi za mwanzo wa ligi kutokana na kutibu majeraha ya kidole ambayo aliyapata kwenye maandalizi ya ligi.”Kwa sasa bado sijaanza kukaa langoni kwa kuwa ninasumbuliwa na maumivu ya kidole ila ninashukuru Mungu ninaendelea vizuri hivi karibuni nitarejea uwanjani,” amesema.Ruvu Shooting imecheza mechi mbili ikiwa ni pamoja na ile ya ufunguzi dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Gairo kwenye sare ya bila kufungana na ya pili ilikuwa Uwanja wa Sokoine wakati ikipokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Ihefu.,

 


NYOTA mpya ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting yenye maskani yake Pwani, Adam Dacosta ameanza na majanga baada ya kuumia kidole.


Dacosta aliibukia ndani ya Ruvu Shooting akitokea Klabu ya Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.

Akizungumza na Saleh Jembe, Dacosta amesema kuwa ameshindwa kucheza mechi za mwanzo wa ligi kutokana na kutibu majeraha ya kidole ambayo aliyapata kwenye maandalizi ya ligi.

“Kwa sasa bado sijaanza kukaa langoni kwa kuwa ninasumbuliwa na maumivu ya kidole ila ninashukuru Mungu ninaendelea vizuri hivi karibuni nitarejea uwanjani,” amesema.

Ruvu Shooting imecheza mechi mbili ikiwa ni pamoja na ile ya ufunguzi dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Gairo kwenye sare ya bila kufungana na ya pili ilikuwa Uwanja wa Sokoine wakati ikipokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Ihefu.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *