Posted By Posted On

SASA NI VITA YA KAGERA SUGAR V YANGA

 BAADA ya Kagera Sugar kumalizana na Gwambina FC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex kibarua chao kinachofuata ni dhidi ya Yanga.Kwenye mchezo wao dhidi ya Gwambina FC dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana na kugawana pointi mojamoja.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba, 19 Uwanja wa Kaitaba,Bukoba na utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza nje ya Dar.Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu hizi mbili zimekuwa na matokeo yasiyotabirika.Mchezo wao wa kwanza msimu uliopita uliochezwa Uwanja wa Uhuru,Kagera Sugar ilishinda mabao 3-0 na ule wa pili Yanga ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Kaitaba.,

 


BAADA ya Kagera Sugar kumalizana na Gwambina FC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex kibarua chao kinachofuata ni dhidi ya Yanga.


Kwenye mchezo wao dhidi ya Gwambina FC dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana na kugawana pointi mojamoja.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba, 19 Uwanja wa Kaitaba,Bukoba na utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza nje ya Dar.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu hizi mbili zimekuwa na matokeo yasiyotabirika.


Mchezo wao wa kwanza msimu uliopita uliochezwa Uwanja wa Uhuru,Kagera Sugar ilishinda mabao 3-0 na ule wa pili Yanga ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.


Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Kaitaba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *