Posted By Posted On

BIASHARA UNITED KAMILI KUMALIZANA NA SIMBA

GERALD Mdamu, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Biashara United amesema kuwa wamejipanga kufanya vema kwenye mechi zao zote za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na ile inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki dhidi ya Simba itakayopigwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa.Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza imeweza kujiwekea kibindoni pointi sita na imefunga mabao mawili baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo.Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Gwambina FC kisha kazi ya mwisho ilikuwa mbele ya Mwadui FC ambapo ilishinda bao 1-0 na mechi zote zilichezwa Uwanja wa Karume, Mara.Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani wa ligi na imani ni kuona kwamba wanaendelea kupata ushindi kwenye mechi zao.”Ligi imeanza kwa ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi, hata sisi pia tunahitaji ushindi kwa mechi zetu zote ambazo tutacheza.”Tunatambua kwamba mchezo wetu ujao ni dhidi ya Simba, tutapambana kupata matokeo chanya, mshabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.Nyota huyo aliibukia ndani ya Biashara United akitokea Klabu ya Mwadui FC ambapo alikuwa kwa msimu wa 2019/20.Biashara United ikiwa imetupia mabao mawili amehusika kwenye pasi moja ya bao ilikuwa mbele ya Gwambina FC wakati ikishinda bao 1-0.,

GERALD Mdamu, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Biashara United amesema kuwa wamejipanga kufanya vema kwenye mechi zao zote za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na ile inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki dhidi ya Simba itakayopigwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa.


Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza imeweza kujiwekea kibindoni pointi sita na imefunga mabao mawili baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo.

Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Gwambina FC kisha kazi ya mwisho ilikuwa mbele ya Mwadui FC ambapo ilishinda bao 1-0 na mechi zote zilichezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani wa ligi na imani ni kuona kwamba wanaendelea kupata ushindi kwenye mechi zao.

“Ligi imeanza kwa ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi, hata sisi pia tunahitaji ushindi kwa mechi zetu zote ambazo tutacheza.

“Tunatambua kwamba mchezo wetu ujao ni dhidi ya Simba, tutapambana kupata matokeo chanya, mshabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.

Nyota huyo aliibukia ndani ya Biashara United akitokea Klabu ya Mwadui FC ambapo alikuwa kwa msimu wa 2019/20.

Biashara United ikiwa imetupia mabao mawili amehusika kwenye pasi moja ya bao ilikuwa mbele ya Gwambina FC wakati ikishinda bao 1-0.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *