Posted By Posted On

HAJI MANARA ALIPA FAINI YA MILION 5 TFF LEO

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba, leo Septemba 16 amelipa faini ya shilingi miloni 5 aliyopigwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho aSoka Tanzania,(TFF). Manara amelipa faini hiyo baada ya kupewa maelekezo ambapo adhabu kama yake ilimkuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli lakini makosa yalikuwa tofauti. Mwingine aliyekutana na adhabu kutoka TFF ni pamoja Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Shirikisho hilo Zakaria Hanspope.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Wakili Kichere Mwita wakati akisoma maamuzi ya kamati dhidi ya Haji Manara alisema kuwa alikutwa na hatia ya kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji wakati wa kesi ya Bernard Morrison kwa maneno aliyotoa kupita Wasafi Media.Taarifa iliyotolewa kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram ya Simba imeeleza kuwa:-Afisa Habari wa klabu, Haji Manara leo mchana amefika kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kulipa faini ya milioni 5 ambayo alipigwa na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.,

 


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba, leo Septemba 16 amelipa faini ya shilingi miloni 5 aliyopigwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho aSoka Tanzania,(TFF).


 Manara amelipa faini hiyo baada ya kupewa maelekezo ambapo adhabu kama yake ilimkuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli lakini makosa yalikuwa tofauti. Mwingine aliyekutana na adhabu kutoka TFF ni pamoja Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Shirikisho hilo Zakaria Hanspope.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Wakili Kichere Mwita wakati akisoma maamuzi ya kamati dhidi ya Haji Manara alisema kuwa alikutwa na hatia ya kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji wakati wa kesi ya Bernard Morrison kwa maneno aliyotoa kupita Wasafi Media.


Taarifa iliyotolewa kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram ya Simba imeeleza kuwa:-Afisa Habari wa klabu, Haji Manara leo mchana amefika kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kulipa faini ya milioni 5 ambayo alipigwa na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *