Posted By Posted On

KINACHOMZUIA KAGERE KUONDOKA SIMBA HIKI HAPA

 PATRICK Gakumba, wakala wa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa amepokea ofa nyingi kutoka timu tofauti zikitaka saini ya mchezaji huyo.Kwa sasa, Kagere amejenga ushkaji mkubwa na benchi kwa msimu wa 2020/21 akiwa hajamaliza dakika 90 ndani ya mechi mbili za ligi ambazo Simba imecheza mpaka sasa.Mechi hizo ni dhidi ya Ihefu FC ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, Kagere alitumia dakika 23 na mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Jamhuri, Kagere alitumia dakika 24.Gakumba amesema:”Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na utaisha mwakani mwezi wa tano. Mpaka sasa tuna ofa nyingi ambazo zinamtaka mapema ili tusaini mkataba wa awali lakini nawaheshimu Simba na wanakidhi mahitaji yake tulivokubaliana.”Kagere ndani ya misimu miwili akiwa Simba amefunga jumla ya mabao 45. Alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na alifunga mabao 22 msimu wa 2019/20.,


 PATRICK Gakumba, wakala wa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa amepokea ofa nyingi kutoka timu tofauti zikitaka saini ya mchezaji huyo.


Kwa sasa, Kagere amejenga ushkaji mkubwa na benchi kwa msimu wa 2020/21 akiwa hajamaliza dakika 90 ndani ya mechi mbili za ligi ambazo Simba imecheza mpaka sasa.

Mechi hizo ni dhidi ya Ihefu FC ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, Kagere alitumia dakika 23 na mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Jamhuri, Kagere alitumia dakika 24.

Gakumba amesema:”Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na utaisha mwakani mwezi wa tano. Mpaka sasa tuna ofa nyingi ambazo zinamtaka mapema ili tusaini mkataba wa awali lakini nawaheshimu Simba na wanakidhi mahitaji yake tulivokubaliana.”

Kagere ndani ya misimu miwili akiwa Simba amefunga jumla ya mabao 45. Alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na alifunga mabao 22 msimu wa 2019/20.,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *