Posted By Posted On

MFUMO MPYA WA BONASI NDANI YA YANGA WABADILIKA

 HERSI Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba wanaendelea kutoa bonasi kwa mtindo wa kipekee tofauti na msimu uliopita.Injinia amesema kuwa kwa sasa ni furaha kubwa kuona timu ikiwa imara na inafanya vizuri baada ya usajili makini jambo linalofanya watu wengi kuifuatilia ligi ikiwa ni pamoja na watu wa Angola kwa kuwa kuna mchezaji ambaye anacheza ndani ya klabu ya Yanga.”Wengi walikuwa hawaitambui ligi ya Tanzania ila kupitia kwa wachezaji ambao wanatoka nje ya nchi wanaitangaza ligi na kuifanya inakuwa kubwa na inafuatiliwa zaidi hili ndilo ambalo tunataka liendelee kufanyika nasi tunapenda. Kuhusu Bonasi amesema”Msimu uliopita tulikuwa na bonasi katika kila mechi ilikuwa ukishinda basi unapata bonasi ila tukishindwa tulikuwa hatutoi pamoja na sare hakukuwa na bonasi, msimu huu tunataka kugawa kutokana na pointi ambazo tutakuwa tunazitaka kwamba katika pointi 15 tunazitafuta pointi.”Lengo ni kuona kwamba katika pointi 15 ikitokea tukapata pointi 10 hapo hela itatolewa na tukipata pointi tano nje ya pointi 15 hapo hakuna sababu ya kupata kitu chochote,” amesema.Chanzo:Azam Tv,

 


HERSI Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba wanaendelea kutoa bonasi kwa mtindo wa kipekee tofauti na msimu uliopita.

Injinia amesema kuwa kwa sasa ni furaha kubwa kuona timu ikiwa imara na inafanya vizuri baada ya usajili makini jambo linalofanya watu wengi kuifuatilia ligi ikiwa ni pamoja na watu wa Angola kwa kuwa kuna mchezaji ambaye anacheza ndani ya klabu ya Yanga.

“Wengi walikuwa hawaitambui ligi ya Tanzania ila kupitia kwa wachezaji ambao wanatoka nje ya nchi wanaitangaza ligi na kuifanya inakuwa kubwa na inafuatiliwa zaidi hili ndilo ambalo tunataka liendelee kufanyika nasi tunapenda. 

Kuhusu Bonasi amesema

“Msimu uliopita tulikuwa na bonasi katika kila mechi ilikuwa ukishinda basi unapata bonasi ila tukishindwa tulikuwa hatutoi pamoja na sare hakukuwa na bonasi, msimu huu tunataka kugawa kutokana na pointi ambazo tutakuwa tunazitaka kwamba katika pointi 15 tunazitafuta pointi.

“Lengo ni kuona kwamba katika pointi 15 ikitokea tukapata pointi 10 hapo hela itatolewa na tukipata pointi tano nje ya pointi 15 hapo hakuna sababu ya kupata kitu chochote,” amesema.


Chanzo:Azam Tv

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *