Posted By Posted On

MO ALIAMSHA DUDE MSIMBAZI

NA WINFRIDA MTOI KUTOKANA na hali inayoendelea katika mitandao ya kijamii, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amecharuka na kusema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaotumia jina lake kumchafua. Hivi karibuni baada ya Mo kuhusishwa kutumia kaunti yake ya twitter kumjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala
The post MO ALIAMSHA DUDE MSIMBAZI appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KUTOKANA na hali inayoendelea katika mitandao ya kijamii, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amecharuka na kusema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaotumia jina lake kumchafua.
Hivi karibuni baada ya Mo kuhusishwa kutumia kaunti yake ya twitter kumjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala ambaye pia ni shabiki wa Simba akihoji kuhusu shilingi bilioni 20 za uwekezaji, kumekuwa na muendelezo wa maneno mbalimbali yanayoandikwa katika akaunti anayodai ni feki ikitumia jina lake.
Hali hiyo imekuwa ikizua taharuki kwa wapenzi na wadau wa klabu hiyo na kuleta mkanganyiko ndani ya Simba, huku wengi wakichukulia maneno hayo ni kweli yanatoka kwa bosi wao huyo.
Kutokana na hali hiyo kukithiri, Mo ameamua kutoa ya moyoni na kusema uvumilivu umemshinda na lazima atachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaotengeneza akaunti feki za kumchafua, yeye na jina la klabu ya Simba.
Katika akaunti zake za mitandaoni jana, Mo aliandika kuwa hahusiki na akaunti hizo zinazoleta taharuki kwa Wanasimba na anafuatilia kwa umakini kujua mhusika wa hilo.
“Hivi karibuni kumeibuka wimbi la akaunti feki za Twitter zikionesha ni zangu na zimekuwa zikitoa taarifa zinazoleta taharuki kwa Wanasimba. Nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa sihusiki nazo.
“Nafuatilia kwa ukaribu kujua ni nani mhusika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake,” aliandika Mo katika mitandao yake ya kijamii.
Aidha aliwasisitiza Wanasimba wasikubali kutolewa katika reli, bali wapambane kuhakikisha klabu yao inafikia mafanikio waliyotarajia.

The post MO ALIAMSHA DUDE MSIMBAZI appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *