Posted By Posted On

SABABU YA MANARA KULIPA MILIONI TANO TFF MAPEMA HII HAPA

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba, amesema kuwa sababu kubwa ya kulipa faini ya milioni tano mapema ni kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).Manara leo Septemba 16 ameripoti makao makuu ya TFF kulipa faini anbayo alitonzwa kutokana na kile kilichoelezwa na Kamati ya Maadili kuwa aliingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison kwa maneno aliyosema kupita Wasafi Media.Manara amesema: “Hatujalipa kwa sababu ya kiburi bali kuheshimu maamuzi ambayo yametolewa na tunaamini kwamba jambo hili litabadili mitazamo ya wengi katika masuala ya mipira, haijalishi tunapitia katika hali gani.”Nimeona kwamba kuna makundi mbalimbali ambayo yalianza kuchangishana kwa ajili ya kunilipia ila katika hili ninapenda kuwaomba mashabiki waache kufanya hivi wasitishe kuchangishana kwa sasa walikuwa wakifanya kwa mapenzi na walijua kwamba nilikuwa nikipambana kwa ajili ya maslahi ya klabu yetu ya Simba.”Uongozi wa Simba unawashukuru sana mashabiki kwa upendo wenu na namna ambavyo mnajitoa lakini ninapenda kusisitiza kwamba tayari tumeshakamilisha malipo leo kwa sababu nimekwenda kulipa baada ya Klabu ya Simba kuona haina haja ya kukata rufaa,” amesema.,

 


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba, amesema kuwa sababu kubwa ya kulipa faini ya milioni tano mapema ni kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).


Manara leo Septemba 16 ameripoti makao makuu ya TFF kulipa faini anbayo alitonzwa kutokana na kile kilichoelezwa na Kamati ya Maadili kuwa aliingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison kwa maneno aliyosema kupita Wasafi Media.


Manara amesema: “Hatujalipa kwa sababu ya kiburi bali kuheshimu maamuzi ambayo yametolewa na tunaamini kwamba jambo hili litabadili mitazamo ya wengi katika masuala ya mipira, haijalishi tunapitia katika hali gani.

“Nimeona kwamba kuna makundi mbalimbali ambayo yalianza kuchangishana kwa ajili ya kunilipia ila katika hili ninapenda kuwaomba mashabiki waache kufanya hivi wasitishe kuchangishana kwa sasa walikuwa wakifanya kwa mapenzi na walijua kwamba nilikuwa nikipambana kwa ajili ya maslahi ya klabu yetu ya Simba.

“Uongozi wa Simba unawashukuru sana mashabiki kwa upendo wenu na namna ambavyo mnajitoa lakini ninapenda kusisitiza kwamba tayari tumeshakamilisha malipo leo kwa sababu nimekwenda kulipa baada ya Klabu ya Simba kuona haina haja ya kukata rufaa,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *