Posted By Posted On

SIMBA KUTESTI TENA KIKOSI LEO

NA WINFRIDA MTOI TIMU ya Simba imeanza kuinolea makali Biashara United ya Mara kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kupigwa Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Mchezo huo utakuwa wa tatu kwa Simba msimu huu, baada ya kujikusanyia pointi nne katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Ihefu
The post SIMBA KUTESTI TENA KIKOSI LEO appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

TIMU ya Simba imeanza kuinolea makali Biashara United ya Mara kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kupigwa Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utakuwa wa tatu kwa Simba msimu huu, baada ya kujikusanyia pointi nne katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Ihefu FC na Mtibwa Sugar.

Katika mechi hizo walizocheza ugenini, Wanamsimbazi hao walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, kwenye Uwanja wa Sokione mkoni Mbeya, kisha kutoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

Kikosi hicho kilirejea Dar es Salaam juzi na wachezaji kupewa mapumziko ya siku moja kabla ya jana jioni kuanza mazoezi mepesi.

Maandalizi rasmi ya mchezo huo wa kwanza nyumbani yanatarajia kuanza leo, ikiwa ni mikakati ya kuchukua pointi tatu na kusaka ushindi wa mabao mengi nyumbani.

Tangu ligi hiyo imeanza Septemba 6 mwaka huu, timu pekee iliyofanikiwa kushinda kwa mabao mengi ni KMC baada ya kuifunga Mbeya City 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi huo, KMC ndiyo inaongoza ligi kwa sasa, hali ambayo haiwaridhishi Wanasimba ambao ndiyo mabingwa watetezi, hivyo wanahitaji kurejea katika anga zao za kufunga mabao mengi.

Matokeo ya sare dhidi ya Mtibwa Sugar ndiyo iliyoharibu harakati za Wanamsimbazi hao za kuanza ligi kwa kasi, lakini sasa wameahidi kuwa mechi za nyumbani ni sehemu pekee wanayotegemea kurudisha furaha kwa mashabiki wao.

Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, ameweka wazi kuwa, baada ya kucheza katika viwanja vigumu ugenini, wanarejea nyumbani kuonesha soka lao walilozoea la burudani.

“Kikosi kimeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wetu ujao dhidi ya Biashara United, huu ni mchezo wetu wa kwanza nyumbani, tutajitahidi kuwapa furaha mashabiki wetu baada ya kutoka kucheza kwenye viwanja vigumu,” alisema.

Alieleza kuwa benchi la ufundi na wachezaji, wanajua kile wanachotakiwa kufanya katika mchezo huo ambao utakuwa mgumu kutokana na timu ya Biashara United kuanza vizuri ligi.

Msemaji wa Simba, Haji Manara, amewataka mashabiki wao kuondoa hofu kufuatia matokeo ya sare na ushindi mwembamba akiwaahidi kuanza kushuhudia dozi kubwa katika mechi zijazo.

Katika mchezo wa mwisho Simba kukutana na Biashara United kwenye uwanja huo, mabingwa hao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

The post SIMBA KUTESTI TENA KIKOSI LEO appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *