Posted By Posted On

UCHEBE AMPOTEZA JUMLAJUMLA SVEN NDANI YA SIMBA

 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amepotezwa mazima na mtangulizi wake wa zamani, Patrick Aussems, ‘Uchebe’ ambaye alimuachia mikoba yake baada ya kupigwa chini msimu wa 2019/20 kwenye mechi mbili za mwanzo ambazo ni sawa na dakika 180.Sven kwenye mechi zake mbili amevuna pointi nne na kushuhudia timu yake ikifunga mabao matatu huku akipotezwa na rekodi iliyowekwa na Uchebe kwenye mechi mbili ambapo alivuna pointi sita na kushuhudia wachezaji wake wakifunga mabao matano.Uchebe alifungua pazia la ligi kwa kumenyana na wajeda, JKT Tanzania, Agosti 29 na alishinda kwa mabao 3-1 kisha mchezo wake wa pili ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Septemba 13 kwa msimu wa 2019/20 zote zilipigwa ndani ya Uwanja wa Uhuru.Tayari Simba imecheza mechi mbili kwa msimu mpya wa 2020/21, ilianza kumenyana na Ihefu, Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na ilishinda kwa mabao 2-1 na mchezo wa pili ililazimisha sare kwa kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri.,


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amepotezwa mazima na mtangulizi wake wa zamani, Patrick Aussems, ‘Uchebe’ ambaye alimuachia mikoba yake baada ya kupigwa chini msimu wa 2019/20 kwenye mechi mbili za mwanzo ambazo ni sawa na dakika 180.

Sven kwenye mechi zake mbili amevuna pointi nne na kushuhudia timu yake ikifunga mabao matatu huku akipotezwa na rekodi iliyowekwa na Uchebe kwenye mechi mbili ambapo alivuna pointi sita na kushuhudia wachezaji wake wakifunga mabao matano.

Uchebe alifungua pazia la ligi kwa kumenyana na wajeda, JKT Tanzania, Agosti 29 na alishinda kwa mabao 3-1 kisha mchezo wake wa pili ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Septemba 13 kwa msimu wa 2019/20 zote zilipigwa ndani ya Uwanja wa Uhuru.

Tayari Simba imecheza mechi mbili kwa msimu mpya wa 2020/21, ilianza kumenyana na Ihefu, Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na ilishinda kwa mabao 2-1 na mchezo wa pili ililazimisha sare kwa kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *