Posted By Posted On

AZAM FC KUIFUATA MBEYA CITY

 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba raia wa Romania leo Septemba 17 kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Azam Complex kabla ya kesho kuifuata Mbeya City, Mbeya.Azam FC ina kibarua cha kumenyana na Mbeya City Septemba 20, na utakuwa mchezo wao wa kwanza nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21.Tayari imecheza mechi mbili kukamilisha mzunguko wa pili na imeshinda zote Uwanja wa Azam Complex ikiwa na mabao matatu kibindoni na pointi zake sita.Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kisha ikamalizana na Coastal Union, kwa ushindi wa mabao 2-0.Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kwa kuwa wameanza vizuri malengo yao nikuendelea na rekodi hiyo.”Tumeanza vizuri mechi zetu za mwanzo ambazo tulikuwa nyumbani, tuna amini tutaendelea na rekodi yetu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.,


 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba raia wa Romania leo Septemba 17 kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Azam Complex kabla ya kesho kuifuata Mbeya City, Mbeya.


Azam FC ina kibarua cha kumenyana na Mbeya City Septemba 20, na utakuwa mchezo wao wa kwanza nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21.

Tayari imecheza mechi mbili kukamilisha mzunguko wa pili na imeshinda zote Uwanja wa Azam Complex ikiwa na mabao matatu kibindoni na pointi zake sita.

Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kisha ikamalizana na Coastal Union, kwa ushindi wa mabao 2-0.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kwa kuwa wameanza vizuri malengo yao nikuendelea na rekodi hiyo.


“Tumeanza vizuri mechi zetu za mwanzo ambazo tulikuwa nyumbani, tuna amini tutaendelea na rekodi yetu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *