Posted By Posted On

BIASHARA UNITED KUKUTANA NA MUZIKI WA MUGALU, BWALYA KWA MKAPA

 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck anatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wa wikiendi ijayo dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kocha huyo anataka kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kukosa ushindi mbele ya Mtibwa Sugar, hivyo atawapa nafasi wachezaji wengi ambao alishindwa kuwatumia mikoani kutokana na ubovu wa viwanja.Rweyemamu aliliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji na benchi la ufundi wanajua kuwa mchezo dhidi ya Biashara ni muhimu kwao, hivyo kocha Sven atabadilisha kikosi kwa kiasi kikubwa kwa kuwa uwanja wanaokwenda kucheza ni mzuri na utawapa nafasi ya kucheza soka lao la siku zote. “Mwalimu amepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chetu, kama ambavyo unafahamu mchezo huu ni muhimu sana kwetu kwa kuwa tunataka kurejesha imani kwa mashabiki wetu. Kila mchezaji na benchi la ufundi wanajua umuhimu wa mchezo huu.“Uwanja ni mzuri baada ya kupambana na viwanja vya mikoani ambavyo siyo rafiki sana. Hapa Dar tutacheza soka letu na watu watafurahi kwa kuwa wachezaji wote mafundi wanaweza wakaanza kwenye mchezo huo,” alisema Rweyemamu. Simba ilishindwa kuwatumia nyota wake wapya wa kikosi hicho, Rally Bwalya na Cris Mugalu katika michezo miwili waliyocheza ugenini, Mbeya dhidi ya Ihefu na Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar. Hivyo wikiendi hii wanatarajia kuwepo kikosini.Mchezo huo utapigwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni.,

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck anatarajia kufanya mabad
iliko makubwa ya wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wa wikiendi ijayo dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kocha huyo anataka kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kukosa ushindi mbele ya Mtibwa Sugar, hivyo atawapa nafasi wachezaji wengi ambao alishindwa kuwatumia mikoani kutokana na ubovu wa viwanja.


Rweyemamu aliliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji na benchi la ufundi wanajua kuwa mchezo dhidi ya Biashara ni muhimu kwao, hivyo kocha Sven atabadilisha kikosi kwa kiasi kikubwa kwa kuwa uwanja wanaokwenda kucheza ni mzuri na utawapa nafasi ya kucheza soka lao la siku zote.

 

“Mwalimu amepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chetu, kama ambavyo unafahamu mchezo huu ni muhimu sana kwetu kwa kuwa tunataka kurejesha imani kwa mashabiki wetu. Kila mchezaji na benchi la ufundi wanajua umuhimu wa mchezo huu.

“Uwanja ni mzuri baada ya kupambana na viwanja vya mikoani ambavyo siyo rafiki sana. Hapa Dar tutacheza soka letu na watu watafurahi kwa kuwa wachezaji wote mafundi wanaweza wakaanza kwenye mchezo huo,” alisema Rweyemamu.

 

Simba ilishindwa kuwatumia nyota wake wapya wa kikosi hicho, Rally Bwalya na Cris Mugalu katika michezo miwili waliyocheza ugenini, Mbeya dhidi ya Ihefu na Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar. Hivyo wikiendi hii wanatarajia kuwepo kikosini.


Mchezo huo utapigwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *