Posted By Posted On

BOSI SIMBA AWAPA WATANI ZAKE MECHI 10

 MMOJA wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hans Poppe, kama ameimpa mechi 10 tu timu ya Yanga ambayo inatamba na kiungo mshambuliaji wao, Carlos Carlinhos. Carlinhos ni kati ya wachezaji gumzo hapa nchini kwa sasa akiwa amefanikiwa kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo mmoja wa ligi aliocheza akiingia akitokea benchi. Wikiendi iliyopita alikuwa gumzo baada ya kuisaidia timu yake ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.Hans Poppe amesema ni mapema mno kuweza kuzungumzia viwango vya timu na wachezaji kwa sasa kwa kuwa hazikwenda katika maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’.Ligi ni ngumu kila timu inahitaji kuona inafanikiwa kufanya vyema huko mbele, lakini ni mapema mno kuweza kutoa tathimini ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwani hakuna ambayo ilikwenda kufanya Pre Season kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi.“Hivyo ni mapema mno kuelewa itakuwaje na nani staa kwa sasa hadi mechi ya 10 huko ndio timu zitaanza kuwa na ushindani na itafahamika nani ni staa na timu gani ni bora, kwa sasa ndiyo maana timu nyingi hazifanyi vizuri,” alisema Hans Poppe.Chanzo: Championi,

 


MMOJA wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hans Poppe, kama ameimpa mechi 10 tu timu ya Yanga ambayo inatamba na kiungo mshambuliaji wao, Carlos Carlinhos.

 

Carlinhos ni kati ya wachezaji gumzo hapa nchini kwa sasa akiwa amefanikiwa kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo mmoja wa ligi aliocheza akiingia akitokea benchi.

 

Wikiendi iliyopita alikuwa gumzo baada ya kuisaidia timu yake ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Hans Poppe amesema ni mapema mno kuweza kuzungumzia viwango vya timu na wachezaji kwa sasa kwa kuwa hazikwenda katika maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’.


Ligi ni ngumu kila timu inahitaji kuona inafanikiwa kufanya vyema huko mbele, lakini ni mapema mno kuweza kutoa tathimini ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwani hakuna ambayo ilikwenda kufanya Pre Season kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi.


“Hivyo ni mapema mno kuelewa itakuwaje na nani staa kwa sasa hadi mechi ya 10 huko ndio timu zitaanza kuwa na ushindani na itafahamika nani ni staa na timu gani ni bora, kwa sasa ndiyo maana timu nyingi hazifanyi vizuri,” alisema Hans Poppe.


Chanzo: Championi

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *