Posted By Posted On

MUANGOLA WA YANGA KUPEWA MKWANJA WA MAANA NA MABOSI

 MABOSI wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga wamefunguka kuwa watawamwagia fedha wachezaji wa kikosi hicho akiwemo Muangola Carlos Carlinhos, kwa ajili ya kuongeza hamasa kuelekea mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Mabosi hao wamepanga kutoa fedha hizo kwa Carlinhos na wenzake kwa ajili ya kuwafanya wapambane na kushinda ili kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu. Kwa mara ya kwanza Carlinhos na mastaa wengine wa Yanga watacheza mechi ya Ligi Kuu Bara nje ya Dar wakipambana na Kagera Sugar Jumamosi hii katika Uwanja wa Kaitaba, Kagera.Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema kuwa watatoa bonasi hiyo kwa kikosi hicho kwa ajili ya kuhamasisha ushindi kama ambavyo walivyofanya kwenye mechi mbili za kwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City. “Mechi ijayo tunataka ushindi tu na hakuna kingine kwa sababu hilo ndiyo lengo letu ili mwisho tuweze kutwaa ubingwa ambao tunautaka kwa msimu huu.“Tutatoa hamasa na bonasi kwa ajili ya wachezaji kufanya vizuri kama ambavyo ilivyokuwa katika mechi zetu za awali za ligi tulivyofanya. “Kikosi chetu kwa sasa kinasaka ‘chemistry’ kwa sababu wachezaji wengi walikuwa hawachezi kama vile Carlinhos. Mechi iliyopita amepata nafasi ya kucheza, aliingia kwa dakika 30, mechi zinazokuja anaweza akapata dakika 45 na nyingine akamaliza kabisa,” alimaliza Hersi.,


 MABOSI wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga wamefunguka kuwa watawamwagia fedha wachezaji wa kikosi hicho akiwemo Muangola Carlos Carlinhos, kwa ajili ya kuongeza hamasa kuelekea mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.

 

Mabosi hao wamepanga kutoa fedha hizo kwa Carlinhos na wenzake kwa ajili ya kuwafanya wapambane na kushinda ili kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu.

 

Kwa mara ya kwanza Carlinhos na mastaa wengine wa Yanga watacheza mechi ya Ligi Kuu Bara nje ya Dar wakipambana na Kagera Sugar Jumamosi hii katika Uwanja wa Kaitaba, Kagera.


Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema kuwa watatoa bonasi hiyo kwa kikosi hicho kwa ajili ya kuhamasisha ushindi kama ambavyo walivyofanya kwenye mechi mbili za kwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

 

“Mechi ijayo tunataka ushindi tu na hakuna kingine kwa sababu hilo ndiyo lengo letu ili mwisho tuweze kutwaa ubingwa ambao tunautaka kwa msimu huu.


“Tutatoa hamasa na bonasi kwa ajili ya wachezaji kufanya vizuri kama ambavyo ilivyokuwa katika mechi zetu za awali za ligi tulivyofanya.

 

“Kikosi chetu kwa sasa kinasaka ‘chemistry’ kwa sababu wachezaji wengi walikuwa hawachezi kama vile Carlinhos. Mechi iliyopita amepata nafasi ya kucheza, aliingia kwa dakika 30, mechi zinazokuja anaweza akapata dakika 45 na nyingine akamaliza kabisa,” alimaliza Hersi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *