Posted By Posted On

SIMBA YAITUMIA BIASHARA UNITED UJUMBE HUU

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa unatambua shauku ya mashabiki wa timu hiyo ni kuona timu inapata ushindi ndicho itakachofanya kwenye mchezo wao dhidi ya Biashara United Uwanja wa Mkapa.Mchezo huo utapigwa Septemba 20 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ambayo timu ya Simba imeyapata hivi karibuni ilipokuwa ugenini.Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Septemba 12 na mchezo wa kwanza uliochezwa Septemba 6 mbele ya Ihefu, Simba ilishinda kwa mabao 2-1.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji wana kila sababu za kupambana kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Biashara United ambao sio wa kuwabeza. “Tunacheza na timu bora na yenye ushindani ambayo ni Biashara United hilo tunalitambua, lakini wachezaji wanajua kwamba wana deni kubwa kwa mashabiki kwenye mechi za ligi hivyo ushindi unahitajika.“Mechi mbili zilizopita ilikuwa wazi kabisa tulicheza kwenye pitchi ambayo haikuwa rafiki kwetu sasa tunarudi nyumbani, tunacheza pale kwa Mkapa eneo ambalo lina ubora wa Simba.“Mbali na kutafuta ushindi wachezaji wana kazi ya kutoa burudani maana mpira wa Simba unajulikana na hicho ndicho tunachokitaka. Pia tuna waomba mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi nne inakutana na Biashara United ambayo ipo nafasi ya nne na pointi sita zote zikiwa zimecheza mechi mbili.,

 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa unatambua shauku ya mashabiki wa timu hiyo ni kuona timu inapata ushindi ndicho itakachofanya kwenye mchezo wao dhidi ya Biashara United Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo utapigwa Septemba 20 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ambayo timu ya Simba imeyapata hivi karibuni ilipokuwa ugenini.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Septemba 12 na mchezo wa kwanza uliochezwa Septemba 6 mbele ya Ihefu, Simba ilishinda kwa mabao 2-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji wana kila sababu za kupambana kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Biashara United ambao sio wa kuwabeza.

 “Tunacheza na timu bora na yenye ushindani ambayo ni Biashara United hilo tunalitambua, lakini wachezaji wanajua kwamba wana deni kubwa kwa mashabiki kwenye mechi za ligi hivyo ushindi unahitajika.

“Mechi mbili zilizopita ilikuwa wazi kabisa tulicheza kwenye pitchi ambayo haikuwa rafiki kwetu sasa tunarudi nyumbani, tunacheza pale kwa Mkapa eneo ambalo lina ubora wa Simba.

“Mbali na kutafuta ushindi wachezaji wana kazi ya kutoa burudani maana mpira wa Simba unajulikana na hicho ndicho tunachokitaka. Pia tuna waomba mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.


Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi nne inakutana na Biashara United ambayo ipo nafasi ya nne na pointi sita zote zikiwa zimecheza mechi mbili.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *