Posted By Posted On

WANA KMC SASA WAANZA KUIVUTIA KASI MWADUI FC

 TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeanza kujiweka tayari kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Septemba 21.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mwadui Complex na utakuwa ni wa kwanza kwa KMC kutoka nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21.Tayari imecheza mechi mbili na kujikusanyia pointi sita sawa na idadi ya mabao ambayo wamefunga ambayo ni sita huku wao wakifungwa bao moja mechi zote ilikuwa Uwanja wa Uhuru.Ilianza mbele ya Mbeya City kwa ushindi wa mabao 4-0 kisha ikamalizana na Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1.Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kabla ya mechi yao dhidi ya Mwadui FC watacheza mechi za kirafiki ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani. Ikiwa na pointi sita inakutana na Mwadui FC ambayo haijaambulia hata pointi kwenye mechi mbili za mwanzo hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani na mgumu kwa timu zote mbili. ,


 TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeanza kujiweka tayari kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Septemba 21.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mwadui Complex na utakuwa ni wa kwanza kwa KMC kutoka nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21.


Tayari imecheza mechi mbili na kujikusanyia pointi sita sawa na idadi ya mabao ambayo wamefunga ambayo ni sita huku wao wakifungwa bao moja mechi zote ilikuwa Uwanja wa Uhuru.


Ilianza mbele ya Mbeya City kwa ushindi wa mabao 4-0 kisha ikamalizana na Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kabla ya mechi yao dhidi ya Mwadui FC watacheza mechi za kirafiki ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani. 


Ikiwa na pointi sita inakutana na Mwadui FC ambayo haijaambulia hata pointi kwenye mechi mbili za mwanzo hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani na mgumu kwa timu zote mbili. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *