Posted By Posted On

KMC YATAMBA KUENDELEZA REKODI ZAKE VPL

OFISA Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 21, Uwanja wa Mwadui Complex.KMC inayoongoza ligi kwa sasa ikiwa na pointi sita itakutana na Mwadui FC ambayo imepoteza mechi zake zote mbili za mwanzo ndani ya ligi.Christina amesema kuwa wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya mbele ya Mwadui ila wamejipanga kuendelea na rekodi yao ndani ya ligi.”Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kuendeleza rekodi zetu tulizoweka. Kikubwa kilichopo kwa sasa ni kupambana kwa wachezaji ili kupata pointi tatu.”Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kuanza kwetu vizuri pia kunachangiwa kwa asilimia kubwa na sapoti yao kwetu,” amesema.Mechi mbili ilizoshinda KMC ilikuwa mbele ya Mbeya City ambao ilishinda kwa mabao 4-0 kisha ikamalizana na Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1, zote Uwanja wa Uhuru.,


OFISA Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 21, Uwanja wa Mwadui Complex.


KMC inayoongoza ligi kwa sasa ikiwa na pointi sita itakutana na Mwadui FC ambayo imepoteza mechi zake zote mbili za mwanzo ndani ya ligi.

Christina amesema kuwa wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya mbele ya Mwadui ila wamejipanga kuendelea na rekodi yao ndani ya ligi.


“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kuendeleza rekodi zetu tulizoweka. Kikubwa kilichopo kwa sasa ni kupambana kwa wachezaji ili kupata pointi tatu.


“Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kuanza kwetu vizuri pia kunachangiwa kwa asilimia kubwa na sapoti yao kwetu,” amesema.


Mechi mbili ilizoshinda KMC ilikuwa mbele ya Mbeya City ambao ilishinda kwa mabao 4-0 kisha ikamalizana na Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1, zote Uwanja wa Uhuru.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *