Posted By Posted On

MAJEMBE MAPYA POLISI TANZANIA NA JKT TANZANIA YAFUNGUA AKAUNTI ZAO

Daruesh Saliboko ingizo jipya ndani ya Polisi Tanzania amefungua akaunti yake ya mabao leo Septemba 18 wakati timu yake ikitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania.Mchezo huo uliochezwa leo Uwanja wa Ushirika Moshi ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo nyota huyo aliyeibukia kikosini hapo akitokea Lipuli alianza kupachika bao dakika ya 32 nje ya 18 kwa guu lake la kulia kwa mpira wa adhabu.   JKT Tanzania iliweka mzani sawa dakika ya 64 kupitia kwa Kelvin Sabato ambaye naye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Kagera Sugar. Timu zote zimegawana pointi mojamoja kwenye mchezo wa leo ambao ni mzunguko wa tatu ndani ya ligi.,


Daruesh Saliboko ingizo jipya ndani ya Polisi Tanzania amefungua akaunti yake ya mabao leo Septemba 18 wakati timu yake ikitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania.


Mchezo huo uliochezwa leo Uwanja wa Ushirika Moshi ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo nyota huyo aliyeibukia kikosini hapo akitokea Lipuli alianza kupachika bao dakika ya 32 nje ya 18 kwa guu lake la kulia kwa mpira wa adhabu.


   JKT Tanzania iliweka mzani sawa dakika ya 64 kupitia kwa Kelvin Sabato ambaye naye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Kagera Sugar. 

Timu zote zimegawana pointi mojamoja kwenye mchezo wa leo ambao ni mzunguko wa tatu ndani ya ligi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *