Posted By Posted On

MKE WA MUANGOLA WA YANGA ALIPAMBA CHAMPIONI

 MKE wa kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos, Katia Carapichoso Carmo ameonyesha kulikubali Gazeti la Championi baada ya juzi kuliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza na ujumbe kwa Lugha ya Kireno. Gazeti la Championi Jumatano la juzi lilitoka likiwa na picha kubwa ya kiungo huyo na habari ya kuonyesha kuwa ameleta mifumo mitatu ndani ya Yanga.Habari hiyo ambayo ilikuwa gumzo mtaani, ilimvutia mrembo huo na kuamua kulichukua gazeti hilo na kuliposti huku akisindikiza kwa maneno ya Kireno akiwa nchini kwao Angola. Mrembo huyo ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na kiungo huyo, baada ya kuweka gazeti hilo alipata wafuasi wengi ambao walionekana kulikubali gazeti hilo na kuonyesha kuwa ndiyo Gazeti Namba Moja la Michezo la Tanzania ambalo linakubalika zaidi Afrika na duniani kwa sasa. Baada ya mwanamama huyo kuposti, masaa 16 baadaye, Carinhos naye aliweka gazeti hilo kwenye ukurasa wake wa insta story.,


 MKE wa kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos, Katia Carapichoso Carmo ameonyesha kulikubali Gazeti la Championi baada ya juzi kuliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza na ujumbe kwa Lugha ya Kireno.

 

Gazeti la Championi Jumatano la juzi lilitoka likiwa na picha kubwa ya kiungo huyo na habari ya kuonyesha kuwa ameleta mifumo mitatu ndani ya Yanga.


Habari hiyo ambayo ilikuwa gumzo mtaani, ilimvutia mrembo huo na kuamua kulichukua gazeti hilo na kuliposti huku akisindikiza kwa maneno ya Kireno akiwa nchini kwao Angola.


 

Mrembo huyo ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na kiungo huyo, baada ya kuweka gazeti hilo alipata wafuasi wengi ambao walionekana kulikubali gazeti hilo na kuonyesha kuwa ndiyo Gazeti Namba Moja la Michezo la Tanzania ambalo linakubalika zaidi Afrika na duniani kwa sasa.

 

Baada ya mwanamama huyo kuposti, masaa 16 baadaye, Carinhos naye aliweka gazeti hilo kwenye ukurasa wake wa insta story.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *