Posted By Posted On

MTIBWA SUGAR YASEPA NA POINTI TATU ZA IHEFU

 MTIBWA Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.Bao pekee la Mtibwa Sugar leo Septemba 18 limepachikwa kwa guu la kushoto na Jaffar Kibaya akiwa ndani ya 18 baada ya mlinda mlango wa Ihefu kutema mpira katika harakati za kuukoa dakika ya 34.Ushindi wa leo ni wa kwanza kwa Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi mbili za ligi, ilianza na Ruvu Shooting ikalazimisha sare ya bila kufungana kisha ikmenyana na Simba na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1.Inafikisha jumla ya pointi tano kibindoni ikiwa imefunga mabao mawili kwenye msimu mpya wa 2020/21.,


 MTIBWA Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao pekee la Mtibwa Sugar leo Septemba 18 limepachikwa kwa guu la kushoto na Jaffar Kibaya akiwa ndani ya 18 baada ya mlinda mlango wa Ihefu kutema mpira katika harakati za kuukoa dakika ya 34.


Ushindi wa leo ni wa kwanza kwa Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi mbili za ligi, ilianza na Ruvu Shooting ikalazimisha sare ya bila kufungana kisha ikmenyana na Simba na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1.


Inafikisha jumla ya pointi tano kibindoni ikiwa imefunga mabao mawili kwenye msimu mpya wa 2020/21.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *