Posted By Posted On

SAMATTA APIGIWA HESABU NA WEST BROM

 IMEELEZWA kuwa Klabu ya West Brom ipo kwenye mpango wa kuipata saini ya nyota wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta.Samatta mwenye umri wa miaka 27 anatajwa pia kuwaniwa na Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ambayo inapewa nafasi kubwa ya kumpata nyota huyo.West Brom itamchukua Samatta kwa mkopo ama kumnunua jumla ikiwa wataelewana kwa upande wa bei na mabosi wake wa Villa.Kwa sasa Samatta bado anapambana akihitaji kubaki ndani ya Ligi Kuu England jambo ambalo linazidi kuonekana kuwa ni gumu kwake kutokana na kushindwa kuonyesha kile ambacho Villa walikitarajia awali.Fernarbahce ina uhitaji mkubwa kwa sasa wakupata mshambuliaji baada ya kumuuza Vedat Muriqi kwenda Lazio hivyo wapo sokoni wakihitaji mbadala wake.Samatta alijiunga na Aston Villa inayonolewa na Kocha Mkuu, Dean Smith akitokea Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Januari kwa dau la pauni milioni 9 baada ya Wesley kuwa na majeraha.Dili lake la miaka minne ndani ya Villa ni mpaka msimu wa 2024.,


 IMEELEZWA kuwa Klabu ya West Brom ipo kwenye mpango wa kuipata saini ya nyota wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta.


Samatta mwenye umri wa miaka 27 anatajwa pia kuwaniwa na Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ambayo inapewa nafasi kubwa ya kumpata nyota huyo.

West Brom itamchukua Samatta kwa mkopo ama kumnunua jumla ikiwa wataelewana kwa upande wa bei na mabosi wake wa Villa.

Kwa sasa Samatta bado anapambana akihitaji kubaki ndani ya Ligi Kuu England jambo ambalo linazidi kuonekana kuwa ni gumu kwake kutokana na kushindwa kuonyesha kile ambacho Villa walikitarajia awali.

Fernarbahce ina uhitaji mkubwa kwa sasa wakupata mshambuliaji baada ya kumuuza Vedat Muriqi kwenda Lazio hivyo wapo sokoni wakihitaji mbadala wake.

Samatta alijiunga na Aston Villa inayonolewa na Kocha Mkuu, Dean Smith akitokea Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Januari kwa dau la pauni milioni 9 baada ya Wesley kuwa na majeraha.

Dili lake la miaka minne ndani ya Villa ni mpaka msimu wa 2024.,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *