Posted By Posted On

SIMBA YAIWEKA KWENYE MIPANGO YANGA MAPEMA

 KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ameelezea malengo yake hivi sasa ni kuhakikisha anashinda michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga. Simba yenye pointi nne sawa na Yanga, zinatarajiwa kuvaana Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara. Kwa mujibu wa Sven, malengo yake ni kushinda michezo hiyo kwa lengo la kukaa kileleni kwenye msimamo ambao hivi sasa wapo KMC wenye pointi sita sawa na Azam FC, Dodoma Jiji FC na Biashara United.Tayari Simba imeshacheza mechi mbili, imeshinda moja na sare moja.Kabla ya kukutana na Yanga, itakuwa tayari imecheza mechi sita.Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema anaamini ana michezo migumu mbele yake, lakini atahakikisha anapambana ili timu yake ipate matokeo mazuri na kuwatoa kileleni KMC. Sven alisema kuwa akishinda michezo hiyo mitano ataanza kupata mwanga wa hatma ya timu yake kuutetea ubingwa wa ligi ambao upo mikononi mwake. “Ninataka kuona timu yangu inapata ushindi wa michezo mitano ijayo ya ligi, ninaamini haitakuwa rahisi lakini nitapambana kufanikisha hilo.“Tayari nimewatahadharisha wachezaji wangu katika hilo kuwa tutakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu. “Hivyo ninataka kuona timu yangu inaongoza ligi kabla ya kukutana na Yanga ili kupunguza presha ya uwajani kwa wachezaji wangu,” alisema Sven. Simba ipo nafasi ya sita huku Yanga ikiwa nafasi ya saba zote zimecheza mechi mbili na kibindoni zina pointi nne.,


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ameelezea malengo yake hivi sasa ni kuhakikisha anashinda michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga.

 

Simba yenye pointi nne sawa na Yanga, zinatarajiwa kuvaana Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Kwa mujibu wa Sven, malengo yake ni kushinda michezo hiyo kwa lengo la kukaa kileleni kwenye msimamo ambao hivi sasa wapo KMC wenye pointi sita sawa na Azam FC, Dodoma Jiji FC na Biashara United.Tayari Simba imeshacheza mechi mbili, imeshinda moja na sare moja.


Kabla ya kukutana na Yanga, itakuwa tayari imecheza mechi sita.Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema anaamini ana michezo migumu mbele yake, lakini atahakikisha anapambana ili timu yake ipate matokeo mazuri na kuwatoa kileleni KMC.

 

Sven alisema kuwa akishinda michezo hiyo mitano ataanza kupata mwanga wa hatma ya timu yake kuutetea ubingwa wa ligi ambao upo mikononi mwake.

 

“Ninataka kuona timu yangu inapata ushindi wa michezo mitano ijayo ya ligi, ninaamini haitakuwa rahisi lakini nitapambana kufanikisha hilo.


“Tayari nimewatahadharisha wachezaji wangu katika hilo kuwa tutakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu.

 

“Hivyo ninataka kuona timu yangu inaongoza ligi kabla ya kukutana na Yanga ili kupunguza presha ya uwajani kwa wachezaji wangu,” alisema Sven. 


Simba ipo nafasi ya sita huku Yanga ikiwa nafasi ya saba zote zimecheza mechi mbili na kibindoni zina pointi nne.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *