Posted By Posted On

SIMBA YATAJA SABABU YA VIINGILIO KUWA BUKU TATU

UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya kuomba viingilio kushushwa kwenye mechi yao dhidi ya Biashara United ni kutaka kuanza sera yao ya kujaza mashabiki kwenye kila mechi ambayo watakuwa wanacheza bila kujali ni wapi.Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa  mipango yao ni kuona kila shabiki na mwanachama wa Simba analipa kiingilio stahiki huku akiipa sapoti timu yake.”Tumepokea taarifa kwa furaha kubwa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania ya kushushwa viingilio hasa kwa upande wa mzunguko kuwa buku tatu,(3000).”Niwaombe mashabiki wa Simba na wanachama pamoja na mashabiki tujae kwa wingi ili tushangilie chama letu. Tumerudi Uwanja wa Mkapa ili kuona namna gani tutashinda na kwa mabao mengi na tunataka tuwe wengi.”Niwakumbushe kuwa mechi itakuwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku, tunataka kuanza kutengeneza utamaduni wa kujaza uwanja katika kila mechi ambazo tutacheza na kutoa burudani,” amesema.Mchezo wa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa utakuwa ni wa kwanza kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi kucheza ndani ya Dar kwa msimu wa 2020/21.Mechi zao mbili zote wamezipiga nje ya Dar, ambapo walianza kumenyana na Ihefu FC Uwanja wa Sokoine Mbeya wakati wakishinda kwa mabao 2-1 ilikuwa Septemba 6.Mchezo wa pili walibanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri, ilikuwa Septemba 12.,

UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya kuomba viingilio kushushwa kwenye mechi yao dhidi ya Biashara United ni kutaka kuanza sera yao ya kujaza mashabiki kwenye kila mechi ambayo watakuwa wanacheza bila kujali ni wapi.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa  mipango yao ni kuona kila shabiki na mwanachama wa Simba analipa kiingilio stahiki huku akiipa sapoti timu yake.

“Tumepokea taarifa kwa furaha kubwa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania ya kushushwa viingilio hasa kwa upande wa mzunguko kuwa buku tatu,(3000).


“Niwaombe mashabiki wa Simba na wanachama pamoja na mashabiki tujae kwa wingi ili tushangilie chama letu. Tumerudi Uwanja wa Mkapa ili kuona namna gani tutashinda na kwa mabao mengi na tunataka tuwe wengi.

“Niwakumbushe kuwa mechi itakuwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku, tunataka kuanza kutengeneza utamaduni wa kujaza uwanja katika kila mechi ambazo tutacheza na kutoa burudani,” amesema.

Mchezo wa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa utakuwa ni wa kwanza kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi kucheza ndani ya Dar kwa msimu wa 2020/21.

Mechi zao mbili zote wamezipiga nje ya Dar, ambapo walianza kumenyana na Ihefu FC Uwanja wa Sokoine Mbeya wakati wakishinda kwa mabao 2-1 ilikuwa Septemba 6.

Mchezo wa pili walibanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri, ilikuwa Septemba 12.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *