Posted By Posted On

TANZANIA PRISONS V NAMUNGO NI VITA YA KISASI

 NAMUNGO FC ina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wao wa kesho, Septemba 19 mbele ya Polisi Tanzania mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Namungo kucheza nje ya Lindi baada ya mechi mbili kutumia uwanja wao wa Majaliwa.Ilianza kumenyana na Coastal Union na ilishinda bao 1-0 kisha ikafungwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kwa kuwa msimu uliopita zilipokutana zilitoana jasho kiasi cha kutosha.Prisons wakati huo ilipokuwa ikitumia Uwanja wa Sokoine, Mbeya ilikubali kufungwa mabao 2-3 kwa mbinde huku ule uliowakutanisha Uwanja wa Majaliwa ngoma ikiwa sare ya kufungana bao 1-1.Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kuyeyusha pointi tatu mazima kwenye mechi zao zilizopita ndani ya ligi.Prisons yenyewe ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Namungo FC ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.,

 


NAMUNGO FC ina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wao wa kesho, Septemba 19 mbele ya Polisi Tanzania mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.


Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Namungo kucheza nje ya Lindi baada ya mechi mbili kutumia uwanja wao wa Majaliwa.


Ilianza kumenyana na Coastal Union na ilishinda bao 1-0 kisha ikafungwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kwa kuwa msimu uliopita zilipokutana zilitoana jasho kiasi cha kutosha.


Prisons wakati huo ilipokuwa ikitumia Uwanja wa Sokoine, Mbeya ilikubali kufungwa mabao 2-3 kwa mbinde huku ule uliowakutanisha Uwanja wa Majaliwa ngoma ikiwa sare ya kufungana bao 1-1.


Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kuyeyusha pointi tatu mazima kwenye mechi zao zilizopita ndani ya ligi.


Prisons yenyewe ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Namungo FC ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *