Posted By Posted On

Baraza: Kiungo ndiyo inaibeba Simba

NA WINFRIDA MTOI WAKATI timu ya Biashara United, ikijipanga kucheza na Simba kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa kikosi hicho, raia wa Kenya Francis Baraza, amesema wapinzani wao wanabebwa zaidi na eneo la viungo, hivyo atahitaji kazi ya ziada kuwadhibiti. Akizungumza na,

NA WINFRIDA MTOI

WAKATI timu ya Biashara United, ikijipanga kucheza na Simba kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa kikosi hicho, raia wa Kenya Francis Baraza, amesema wapinzani wao wanabebwa zaidi na eneo la viungo, hivyo atahitaji kazi ya ziada kuwadhibiti.

Akizungumza na BINGWA jana baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Baraza  alisema siku zote ubora wa Simba unatokana na viungo wengi wanaocheza kwa pamoja.

“Mfumo wa Simba wanaocheza ipo vizuri sana katika kiungo, inatakiwa kuwa makini unapocheza nayo kwa sababu  ina viungo wenye ubora na kufanya mashambulizi,” alisema Baraza.

Baraza alisema katika mchezo huo ataingia kwa tahadhari kubwa akijua anakutana na  bingwa anayetaka kutetea taji lake kwa msimu wa nne mfululizo.

“Tupo  Dar es Salaam, tunafanya maandalizi mazuri, najua mchezo utakuwa mgumu, lakini wachezaji wangu wameonesha ari kuwa wapo tayari kupambana,” kocha huyo.

Biashara United walianza ligi hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina katika mchezo uliochezwa Septemba 7, mwaka huu, kabla ya kupata ushindi kama huo dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma, mkoani  Mara,

Nao Simba walianza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu katika mchezo uliochezwa Septemba 7, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Soikone, jijini Mbeya na baadaye sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar Jumamosi iliyopita katika dimba la Jamhuri, mjini Morogoro.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *