Posted By Posted On

KASI HII IKIENDELEA VPL ITAPENDEZA

 LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, inaendelea kuchanja mbuga ambapo sasa tupo kwenye mzunguko wa tatu baada ya msimu kufunguliwa Septemba 6, mwaka huu. Kila timu inaendelea kuvuna kile ambacho ilipanda kutokana na aina ya matokeo ambayo yanaendelea kupatikana ndani ya uwanja. Bado sijaanza kusikia malalamiko ya timu kuonewa ingawa kuna waamuzi wanaonekana kuanza kuboronga mapema. Mpaka sasa, nimeona kuona tofauti kubwa ya msimu huu na ule uliopita hasa kutoka kwa watendaji wanaosimamia ligi hiyo. Hapa nawalenga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB). Tofauti hiyo ni ile ambayo msimu uliopita ilikuwa ikipigiwa kelele nyingi na wafuatiliaji wa ligi hiyo. Nimeona kuna hatua za haraka zinachukuliwa kwa wale ambao wanatenda makossa. Hii ni tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ambapo wengi walikuwa wakilalamika kwamba makossa yanatendeka, adhabu zinachelewa kutoka. Nianze kwa kuzungumzia ishu ya viwanja, kulikuwa na malalamiko juu ya viwanja ambavyo vinatumika kwa baadhi ya timu kuonekana havina ubora. Mapema sana hata hatujafika mbali, viwanja hivyo vimefungiwa na kutakiwa kufanyiwa maboresho kutokana na kuwa na mapungufu kadhaa. Viwanja vilivyofungiwa ni Gwambina uliopo mkoani Mwanza ukitumiwa na Gwambina FC na Karume unaopatikana Mara ambao unatumika na Biashara United. Zimetolewa siku za kufanyiwa maboresho, kama zikishindwa basi zitaendelea kutumia viwanja vingine vilivyoainishwa kwa mechi zao za nyumbani ambavyo ni CCM Kirumba na Nyamagana vilivyopo Mwanza. Niseme tu kwamba, uwanja ukiwa mbovu hata ile ladha ya mpira nayo inakuwa mbovu kwani mpira hautulii sehemu moja unakuwa ni mwendo wa kukimbizana tu. Kitu kizuri ikiwa maboresho yatafanyika italeta ushindani mkubwa na kila mmoja atapenda kushuhudia mechi zitakavyokuwa zikipigwa kwa ushindani mkubwa. Kuwa na viwanja bora kunafanya ligi nayo kuwa bora kwa sababu wachezaji wanaonesha uwezo wao ule ambao tunautarajia kutoka kwao. Ukiangalia ligi yetu ina wachezaji wa aina mbalimbali kutoka mataifa tofauti. Wengi wao wanashindwa kuonesha ubora wao kwa sababu ya ubovu wa viwanja. Sasa tukiwa na viwanja bora, inakuwa rahisi kwa wao kutupa tunachohitaji. Pia nimependezwa na namna ambavyo adhabu zimetoka haraka kwa waliofanya makosa. Adhabu zimetoka kwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya TFF, Zakaria Hanspope. Hawa wote wamekutwa na makosa mbalimbali katika ile kesi ya kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Morrison. Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, ndiyo iliwaadhibu viongozi hao kwa kulipa faini ya Sh. milioni tano kila mmoja. Pia juzi kuna timu na viongozi wamepewa onyo baada ya kuonekana katika mechi za raundi ya pili kuboronga. Miongoni mwa timu hizo ni Namungo, Mtibwa, Dodoma Jiji na JKT Tanzania. Kasi hii ikiendelea hivi, nauona msimu huu ukiwa wa tofauti sana na ile iliyopita, hapo ushindani utaongezeka zaidi.,

 

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, inaendelea kuchanja mbuga ambapo sasa tupo kwenye mzunguko wa tatu baada ya msimu kufunguliwa Septemba 6, mwaka huu.

 

Kila timu inaendelea kuvuna kile ambacho ilipanda kutokana na aina ya matokeo ambayo yanaendelea kupatikana ndani ya uwanja. Bado sijaanza kusikia malalamiko ya timu kuonewa ingawa kuna waamuzi wanaonekana kuanza kuboronga mapema.

 

Mpaka sasa, nimeona kuona tofauti kubwa ya msimu huu na ule uliopita hasa kutoka kwa watendaji wanaosimamia ligi hiyo. Hapa nawalenga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

 

Tofauti hiyo ni ile ambayo msimu uliopita ilikuwa ikipigiwa kelele nyingi na wafuatiliaji wa ligi hiyo.

 

Nimeona kuna hatua za haraka zinachukuliwa kwa wale ambao wanatenda makossa. Hii ni tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ambapo wengi walikuwa wakilalamika kwamba makossa yanatendeka, adhabu zinachelewa kutoka.

 

Nianze kwa kuzungumzia ishu ya viwanja, kulikuwa na malalamiko juu ya viwanja ambavyo vinatumika kwa baadhi ya timu kuonekana havina ubora.

 

Mapema sana hata hatujafika mbali, viwanja hivyo vimefungiwa na kutakiwa kufanyiwa maboresho kutokana na kuwa na mapungufu kadhaa.

 

Viwanja vilivyofungiwa ni Gwambina uliopo mkoani Mwanza ukitumiwa na Gwambina FC na Karume unaopatikana Mara ambao unatumika na Biashara United.

 

Zimetolewa siku za kufanyiwa maboresho, kama zikishindwa basi zitaendelea kutumia viwanja vingine vilivyoainishwa kwa mechi zao za nyumbani ambavyo ni CCM Kirumba na Nyamagana vilivyopo Mwanza.

 

Niseme tu kwamba, uwanja ukiwa mbovu hata ile ladha ya mpira nayo inakuwa mbovu kwani mpira hautulii sehemu moja unakuwa ni mwendo wa kukimbizana tu.

 

Kitu kizuri ikiwa maboresho yatafanyika italeta ushindani mkubwa na kila mmoja atapenda kushuhudia mechi zitakavyokuwa zikipigwa kwa ushindani mkubwa.

 

Kuwa na viwanja bora kunafanya ligi nayo kuwa bora kwa sababu wachezaji wanaonesha uwezo wao ule ambao tunautarajia kutoka kwao.

 

Ukiangalia ligi yetu ina wachezaji wa aina mbalimbali kutoka mataifa tofauti. Wengi wao wanashindwa kuonesha ubora wao kwa sababu ya ubovu wa viwanja.

 

Sasa tukiwa na viwanja bora, inakuwa rahisi kwa wao kutupa tunachohitaji.

 

Pia nimependezwa na namna ambavyo adhabu zimetoka haraka kwa waliofanya makosa. Adhabu zimetoka kwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya TFF, Zakaria Hanspope.

 

Hawa wote wamekutwa na makosa mbalimbali katika ile kesi ya kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Morrison.

 

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, ndiyo iliwaadhibu viongozi hao kwa kulipa faini ya Sh. milioni tano kila mmoja.

 

Pia juzi kuna timu na viongozi wamepewa onyo baada ya kuonekana katika mechi za raundi ya pili kuboronga. Miongoni mwa timu hizo ni Namungo, Mtibwa, Dodoma Jiji na JKT Tanzania.

 

Kasi hii ikiendelea hivi, nauona msimu huu ukiwa wa tofauti sana na ile iliyopita, hapo ushindani utaongezeka zaidi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *