Posted By Posted On

KIUNGO CHIPUKIZI WA AZAM FC AVUKA HATUA YA KWANZA YA MAJARIBIO YA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA ISRAEL

Na Mwandsh Wetu, DAR ES SALAAMKIUNGO chipukizi wa Azam FC, Novatus Dismas, anaendelea vyema na majaribio yake katika klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Israel baada ya kuanza kuivutia timu hiyo.Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Maccabi ilituma mwaliko wa mafunzo Azam FC ikimuomba Mchezaji huyo Bora Chipukizi wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili kumfanyia majaribio kwa siku 20.Mara baada ya nyota huyo kuwavutia mazoezini akiwa na kikosi cha timu ya vijana Maccabi U-20, walimbadilishia programu kutoka mafunzo hadi majaribio kamili.Novatus Dismas, anaendelea vyema na majaribio yake Maccabi Tel Aviv ya Israel Akiwa amemaliza wiki ya kwanza, tayari Novatus ameshacheza mchezo mmoja wa kirafiki akiwa na timu ya vijana, ambapo anatarajia kumalizia majaribio yake kwa kucheza mechi nyingine mbili za kirafiki.Aidha mara baada ya mechi hizo, Maccabi inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, inatarajia kutoa ripoti kamili ya nyota huyo, huku matarajio makubwa yakiwa ni kijana huyo kununuliwa kutoka Azam FC. ,

Na Mwandsh Wetu, DAR ES SALAAM

KIUNGO chipukizi wa Azam FC, Novatus Dismas, anaendelea vyema na majaribio yake katika klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Israel baada ya kuanza kuivutia timu hiyo.

Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Maccabi ilituma mwaliko wa mafunzo Azam FC ikimuomba Mchezaji huyo Bora Chipukizi wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili kumfanyia majaribio kwa siku 20.

Mara baada ya nyota huyo kuwavutia mazoezini akiwa na kikosi cha timu ya vijana Maccabi U-20, walimbadilishia programu kutoka mafunzo hadi majaribio kamili.

Novatus Dismas, anaendelea vyema na majaribio yake Maccabi Tel Aviv ya Israel 

Akiwa amemaliza wiki ya kwanza, tayari Novatus ameshacheza mchezo mmoja wa kirafiki akiwa na timu ya vijana, ambapo anatarajia kumalizia majaribio yake kwa kucheza mechi nyingine mbili za kirafiki.

Aidha mara baada ya mechi hizo, Maccabi inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, inatarajia kutoa ripoti kamili ya nyota huyo, huku matarajio makubwa yakiwa ni kijana huyo kununuliwa kutoka Azam FC. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *