Posted By Posted On

KOCHA YANGA AMPA MUDA YACOUBA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ameibuka na kumkingia kifua straika wake, Yacouba Songne kwa kusema kuwa anahitaji muda kwa ajili ya kuonyesha uwezo wake. Mserbia huyo ameongeza kuwa kwa sasa straika wake huyo anaendelea kuwa sawa kutokana na kukaa zaidi ya miezi mitano bila ya kucheza mpira kutokana na suala la Virusi vya Corona.Yacouba ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Asante Kotoko ya Ghana hadi sasa ameshacheza mechi mbili akiwa na klabu hiyo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku akishindwa kufunga bao lolote. Krmpotic amesema kuwa hawezi kumlaumu straika huyo kwa kushindwa kufunga katika mechi hizo kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila ya kucheza kutokana na ligi yao kusimama kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona. “Yacouba hajacheza kwa miezi mitano iliyopita kwa sababu ya Corona, siyo rahisi kuonyesha kiwango kikubwa kwa kipindi hiki ambacho anacheza kwa sasa. “Lakini pia amefika hapa wiki chache nyuma ndiyo akaanza mazoezi na wenzake. Namuandaa kuja kuwa hatari kwa siku zijazo pale ambapo atakaa sawa na kuelewana na wenzake ndani ya timu,” alimaliza Mserbia huyo.,


KOCHA Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ameibuka na kumkingia kifua straika wake, Yacouba Songne kwa kusema kuwa anahitaji muda kwa ajili ya kuonyesha uwezo wake.

 

Mserbia huyo ameongeza kuwa kwa sasa straika wake huyo anaendelea kuwa sawa kutokana na kukaa zaidi ya miezi mitano bila ya kucheza mpira kutokana na suala la Virusi vya Corona.


Yacouba ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Asante Kotoko ya Ghana hadi sasa ameshacheza mechi mbili akiwa na klabu hiyo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku akishindwa kufunga bao lolote.

 

Krmpotic amesema kuwa hawezi kumlaumu straika huyo kwa kushindwa kufunga katika mechi hizo kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila ya kucheza kutokana na ligi yao kusimama kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

 

“Yacouba hajacheza kwa miezi mitano iliyopita kwa sababu ya Corona, siyo rahisi kuonyesha kiwango kikubwa kwa kipindi hiki ambacho anacheza kwa sasa.

 

“Lakini pia amefika hapa wiki chache nyuma ndiyo akaanza mazoezi na wenzake. Namuandaa kuja kuwa hatari kwa siku zijazo pale ambapo atakaa sawa na kuelewana na wenzake ndani ya timu,” alimaliza Mserbia huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *