Posted By Posted On

MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC PRINCE KUONJA JOTO YA JIWE

 PRINCE Dube, nyota wa Klabu ya Azam FC ambaye amehusika kwenye mabao matatu kati ya matatu ambayo yamefungwa na timu hiyo kuanza kuonja joto ya jiwe Septemba 20 kwa kucheza muda tofauti na aliozoea.Nyota huyo ana mabao mawili ambayo aliifungia timu yake wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na ana pasi moja ya bao aliyompa Obrey Chirwa wakati Azam FC ikishinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.Mechi zote ambazo Prince alifunga na kutoa pasi zilichezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku anakwenda kuonja joto ya jiwe na muziki wa saa 8:00 mchana Mbeya Uwanja wa Sokoine.Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ameliambia Championi Jumamosi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi zao zote kwa kuwa wamejipanga.Azam FC inakutana na Mbeya City ambayo imeyeyusha pointi sita kwenye mechi zake mbili ilizocheza Dar, mbele ya KMC ilifungwa mabao 4-0 kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.,

 


PRINCE Dube, nyota wa Klabu ya Azam FC ambaye amehusika kwenye mabao matatu kati ya matatu ambayo yamefungwa na timu hiyo kuanza kuonja joto ya jiwe Septemba 20 kwa kucheza muda tofauti na aliozoea.

Nyota huyo ana mabao mawili ambayo aliifungia timu yake wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na ana pasi moja ya bao aliyompa Obrey Chirwa wakati Azam FC ikishinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania.

Mechi zote ambazo Prince alifunga na kutoa pasi zilichezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku anakwenda kuonja joto ya jiwe na muziki wa saa 8:00 mchana Mbeya Uwanja wa Sokoine.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ameliambia Championi Jumamosi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi zao zote kwa kuwa wamejipanga.

Azam FC inakutana na Mbeya City ambayo imeyeyusha pointi sita kwenye mechi zake mbili ilizocheza Dar, mbele ya KMC ilifungwa mabao 4-0 kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *