Posted By Posted On

Mtibwa Sugar yaona mwezi, Polisi, JKT Tanzania sare

WAANDISHI WETU  TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza baada ya kuifunga Ihefu bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Bao la pekee  la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 35 na Jaffar Kibaya. Mtibwa Sugar waliingia uwanjani wakiwa na hamu ya kusaka ushindi baada ya,

WAANDISHI WETU 

TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza baada ya kuifunga Ihefu bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao la pekee  la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 35 na Jaffar Kibaya.

Mtibwa Sugar waliingia uwanjani wakiwa na hamu ya kusaka ushindi baada ya kupoteza pointi nne katika mchezo miwili waliyokuwa wamecheza.

Kwa ushindi huo Mtibwa Sugar imefikisha pointi tano na kushika nafasi ya tano katika msimamo wa  ligi hiyo.

Ihefu ambayo ilijitahidi kufanya mashambulizi katika mchezo huo ilikosa nafasi nyingi za kufunga na kubaki na pointi tatu, baada ya kushuka dimbani mara tatu.

Katika mchezo mwingine, timu  ya Polisi Tanzania imeshindwa kuibuka na ushindi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani hapa.

Polisi Tanzania walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 32, lililofungwa na Darueshi Saliboko dakika 32, kabla ya JKT Tanzania kusawazisha dakika ya 64 kupitia kwa Kevin Sabato.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa kikosi cha Polisi Tanzania, George Mketo, alisema matokeo yamewaumiza kutokana na kuambulia pointi moja.

Mketo alisema watahakikisha wanafanyia kazi kasoro zilizojitokeza ili waweze kushinda mchezo utakaofuata dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Septemba 26, mwaka huu.

Alisema katika mchezo huo  watahakikisha wanapambana ili waweze kupata pointi tatu kwenye wanja wao wa nyumbani wa Ushirika Moshi. 

Kwa upande wake, Kocha wa timu ya JKT Tanzania, Mohamed Abdallah Bares, alisema matokeo siyo mazuri, lakini wamefurahia kupata pointi moja ugenini. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *