Posted By Posted On

SARPONG, MUANGOLA WA YANGA WAINGIA KWENYE MTEGO HUU MAZIMA

MICHAEL Sarpong, mshambuliaji ndani ya Klabu ya Yanga pamoja na kiungo Muangola, Carlos Carlinhos wameingia kwenye mtengo wa kwanza mazima ndani ya kikosi hicho kwa muda wa dakika 180.Sarpong mwili jumba, mwenye bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara ambalo aliwatungua Tanzania Prisons ndani ya 18, Carlinhos kipenzi cha mashabiki mwenye pasi moja ya bao kwa mara ya kwanza watacheza mechi zao za ligi nje ya Dar.Mtego wa kwanza ambao wataingia leo ni wa dakika 90 mbele ya Kagera Sugar kisha Septemba 27 watamaliza dakika 90 mbele ya Mtibwa Sugar, kabla ya kurejea tena Dar kuendeleza mbio za kusaka pointi tatu muhimu. Mechi hizi mbili za viwanja vya nje zimekuwa ni tatizo kwa nyota wengi wakigeni kuonyesha makeke yao hivyo ikiwa watapeta kwenye mechi hizi watakuwa wamevuka kiunzi cha sababu ya mechi za mkoani.Mbali na Sarpong pamoja na Carlinhos nyota wengine wa Yanga ambao watakuwa nje ya Dar kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ni pamoja na Yacouba Sogne,Tuisila Kisinda,Tonombe Mukoko.Ikimalizana na mechi hizo mbili Yanga, itarejea Dar kumenyana na Polisi Tanzania itakuwa Oktoba 11 kisha itakutana na Simba, Oktoba 18, zote Uwanja wa Mkapa.,


MICHAEL Sarpong, mshambuliaji ndani ya Klabu ya Yanga pamoja na kiungo Muangola, Carlos Carlinhos wameingia kwenye mtengo wa kwanza mazima ndani ya kikosi hicho kwa muda wa dakika 180.

Sarpong mwili jumba, mwenye bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara ambalo aliwatungua Tanzania Prisons ndani ya 18, Carlinhos kipenzi cha mashabiki mwenye pasi moja ya bao kwa mara ya kwanza watacheza mechi zao za ligi nje ya Dar.

Mtego wa kwanza ambao wataingia leo ni wa dakika 90 mbele ya Kagera Sugar kisha Septemba 27 watamaliza dakika 90 mbele ya Mtibwa Sugar, kabla ya kurejea tena Dar kuendeleza mbio za kusaka pointi tatu muhimu.

 

Mechi hizi mbili za viwanja vya nje zimekuwa ni tatizo kwa nyota wengi wakigeni kuonyesha makeke yao hivyo ikiwa watapeta kwenye mechi hizi watakuwa wamevuka kiunzi cha sababu ya mechi za mkoani.

Mbali na Sarpong pamoja na Carlinhos nyota wengine wa Yanga ambao watakuwa nje ya Dar kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ni pamoja na Yacouba Sogne,Tuisila Kisinda,Tonombe Mukoko.

Ikimalizana na mechi hizo mbili Yanga, itarejea Dar kumenyana na Polisi Tanzania itakuwa Oktoba 11 kisha itakutana na Simba, Oktoba 18, zote Uwanja wa Mkapa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *