Posted By Posted On

TRENT AMPA SAPOTI NYOTA MWENZAKE ROBERTSON

 BEKI Trent Alexander-Arnold wa Klabu ya Liverpool ameonekana akimpigia debe mchezaji mwenzake  Andy Robertson baada ya kuonesha vitabu vyake vipya kwenye gari yake huku akiwataka wanaohitaji kitabu hicho waweze kujipatia nakala zao mapema.Nyota huyo mwenye miaka 21 kupitia ukurasa wake wa Twitter alitupia picha ya gari lake ikiwa na vitabu vya mchezaji mwenzake ndani ya timu ya Liverpool. Trent kwenye msimu uliopita wakati timu yake ikitwaa taji la Ligi Kuu England alitoa jumla ya pasi 15 na Robertson alitoa jumla ya pasi 12.Nyota huyo wa England amesema kuwa kwa sasa anafurahia kusoma kitabu na historia ya mchezaji mwenzake jambo ambalo amewataka na mashabiki wake waweze kufanya hivyo kwa kupata nakala ili kuelewa historia ya nyota huyo.”Kila kitu kuhusu mauzo ya kitabu cha Robbo ni muhimu kuungwa mkono, amepambana na leo kila kitu kipo kwenye kitabu chake,” amesema.,


 BEKI Trent Alexander-Arnold wa Klabu ya Liverpool ameonekana akimpigia debe mchezaji mwenzake  Andy Robertson baada ya kuonesha vitabu vyake vipya kwenye gari yake huku akiwataka wanaohitaji kitabu hicho waweze kujipatia nakala zao mapema.

Nyota huyo mwenye miaka 21 kupitia ukurasa wake wa Twitter alitupia picha ya gari lake ikiwa na vitabu vya mchezaji mwenzake ndani ya timu ya Liverpool.

 Trent kwenye msimu uliopita wakati timu yake ikitwaa taji la Ligi Kuu England alitoa jumla ya pasi 15 na Robertson alitoa jumla ya pasi 12.

Nyota huyo wa England amesema kuwa kwa sasa anafurahia kusoma kitabu na historia ya mchezaji mwenzake jambo ambalo amewataka na mashabiki wake waweze kufanya hivyo kwa kupata nakala ili kuelewa historia ya nyota huyo.

“Kila kitu kuhusu mauzo ya kitabu cha Robbo ni muhimu kuungwa mkono, amepambana na leo kila kitu kipo kwenye kitabu chake,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *