Posted By Posted On

AZAM FC KIKAANGONI NDANI YA DAKIKA 180

 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Aristica Cioaba leo kina kazi ya kuanza kuzimega dakika 180 za moto ugenini baada ya kuzitumia dakika 90 ndani ya Uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex.Cioaba ataanza kazi ya kwanza  leo mbele ya Mbeya City ambayo ina uchungu wa kuyeyusha pointi sita kwenye mechi zake mbili za ugenini ndani ya ligi.Ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 mbele ya KMC kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga. Azam FC wao walishinda mechi zote mbili ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0 kisha ikamalizana na Coastal Union kwa mabao 2-0.Baada ya kazi ya leo kumalizika mbele ya Mbeya City ina kibarua kingine mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa itakuwa ni Septemba 26.Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ushindani utakuwa mkubwa ila wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi. Azam FC kibindoni ina pointi sita ikiwa nafasi ya tatu ambapo inaanza kumenyana na Mbeya City leo Septemba 20 iliyo nafasi ya 18 ikiwa haijaambulia pointi kwenye mechi zake mbili.,


 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Aristica Cioaba leo kina kazi ya kuanza kuzimega dakika 180 za moto ugenini baada ya kuzitumia dakika 90 ndani ya Uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex.

Cioaba ataanza kazi ya kwanza  leo mbele ya Mbeya City ambayo ina uchungu wa kuyeyusha pointi sita kwenye mechi zake mbili za ugenini ndani ya ligi.

Ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 mbele ya KMC kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga. Azam FC wao walishinda mechi zote mbili ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0 kisha ikamalizana na Coastal Union kwa mabao 2-0.

Baada ya kazi ya leo kumalizika mbele ya Mbeya City ina kibarua kingine mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa itakuwa ni Septemba 26.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ushindani utakuwa mkubwa ila wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi. 

Azam FC kibindoni ina pointi sita ikiwa nafasi ya tatu ambapo inaanza kumenyana na Mbeya City leo Septemba 20 iliyo nafasi ya 18 ikiwa haijaambulia pointi kwenye mechi zake mbili.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *