Posted By Posted On

HASSAN KESSY KAMILI KUKUTANA NA MUZIKI WA SARPONG

 HASSAN Kessy, beki kisiki ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar kwa sasa yupo kamili gado kuuvaa muziki wa Michael Sarpong, mshambuliaji wa Yanga ambaye  amekuwa ni tegemeo ndani ya kikosi hicho.Kessy ambaye ni ingizo jipya ndani ya Mtibwa Sugar akitokea Klabu ya Nkana ya Zambia ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia kwa sasa ni mali ya Mtibwa Sugar ambapo amesaini dili la miaka miwili.Kwenye mechi mbili alikosekana ilikuwa ni mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo wakati Mtibwa Sugar ikilazimisha sare ya bila kufungana kisha mbele ya Simba kwenye sare ya kufungana bao 1-1 hakuwa sehemu ya kikosi, Septemba 18 alikiamsha wakati timu yake ikishinda bao 1-0 mbele ya Ihefu Uwanja wa Sokoine Mbeya.Kessy ameshiriki kwenye ushindi wa kwanza wa timu yake mpya na Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila alisema kuwa anaamini kikosi chake kitaendelea kupambana kupata pointi tatu kwenye mechi zake zinazofuata.Kwa sasa Mtibwa Sugar imeshamalizana na mzunguko wa tatu inaisubiri Yanga ambayo jana ilikuwa inamenyana na Kagera Sugar, mchezo utakaochezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.  Zitakutana Uwanja wa Jamhuri zikiwa zimetoka kushinda mechi zao zilizopita.Yanga ilishinda kwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na kuifanya ifikishe pointi saba ikiwa kileleni baada ya kusepa na pointi tatu za Kagera Sugar jumlajumla. Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Tonombe Mukoko kwa krosi ya Tuisila Kisinda hivyo wageni wa Yanga ikiwa ni pamoja Sarpong wametupia bao mojamoja.,

 


HASSAN Kessy, beki kisiki ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar kwa sasa yupo kamili gado kuuvaa muziki wa Michael Sarpong, mshambuliaji wa Yanga ambaye  amekuwa ni tegemeo ndani ya kikosi hicho.

Kessy ambaye ni ingizo jipya ndani ya Mtibwa Sugar akitokea Klabu ya Nkana ya Zambia ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia kwa sasa ni mali ya Mtibwa Sugar ambapo amesaini dili la miaka miwili.

Kwenye mechi mbili alikosekana ilikuwa ni mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo wakati Mtibwa Sugar ikilazimisha sare ya bila kufungana kisha mbele ya Simba kwenye sare ya kufungana bao 1-1 hakuwa sehemu ya kikosi, Septemba 18 alikiamsha wakati timu yake ikishinda bao 1-0 mbele ya Ihefu Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kessy ameshiriki kwenye ushindi wa kwanza wa timu yake mpya na Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila alisema kuwa anaamini kikosi chake kitaendelea kupambana kupata pointi tatu kwenye mechi zake zinazofuata.

Kwa sasa Mtibwa Sugar imeshamalizana na mzunguko wa tatu inaisubiri Yanga ambayo jana ilikuwa inamenyana na Kagera Sugar, mchezo utakaochezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.  Zitakutana Uwanja wa Jamhuri zikiwa zimetoka kushinda mechi zao zilizopita.


Yanga ilishinda kwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na kuifanya ifikishe pointi saba ikiwa kileleni baada ya kusepa na pointi tatu za Kagera Sugar jumlajumla. 

Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Tonombe Mukoko kwa krosi ya Tuisila Kisinda hivyo wageni wa Yanga ikiwa ni pamoja Sarpong wametupia bao mojamoja.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *