Posted By Posted On

ISHU YA KAGERE NA SVEN IMEFIKIA HAPA

 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Vandebroeck amesema kinachoendelea juu yake na mshambuliaji Meddie Kagere ni siri yake hawezi kuweka hadharani. Sven amedai kuwa kumuanzisha benchi mfungaji bora aliyefunga magoli zaidi ya ishirini kwa misimu miwili mfululizo ni jambo la kawaida. ”Masuala yangu na Meddie Kagere ni siri yangu siwezi kuyasema, kufunga mabao zaidi ya 20 haina maana kwamba anapaswa kuanza kwenye kikosi cha kwanza  kwani Gonzalo Higuain mbona anakaa benchi japo alifunga magoli 30 na ni mshambuliaji bora?. Leo Simba ina kibarua cha kumenyana na Biashara United kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa. Kagere amekuwa hana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 kwenye ligi ambapo kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 ametumia dakika 47. Alianza kusugua benchi mbele ya Ihefu FC wakati Simba ikishinda mabao 3-2 akitumia dakika 23 kisha mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 aliyeyusha dakika 24.Kwa misimu miwili mfululizo Kagere amekuwa ni mfungaji bora ndani ya ligi ambapo aliibuka mfungaji bora msimu wa 2018/19 alipofunga mabao 23 kisha 2019/20 alifunga mabao 22.Ndani ya misimu yake miwili akiwa Bongo, Kagere raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao 45 kwenye ligi pekee.,

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Vandebroeck amesema kinachoendelea juu yake na mshambuliaji Meddie Kagere ni siri yake hawezi kuweka hadharani.

 

Sven amedai kuwa kumuanzisha benchi mfungaji bora aliyefunga magoli zaidi ya ishirini kwa misimu miwili mfululizo ni jambo la kawaida.

 

”Masuala yangu na Meddie Kagere ni siri yangu siwezi kuyasema, kufunga mabao zaidi ya 20 haina maana kwamba anapaswa kuanza kwenye kikosi cha kwanza  kwani Gonzalo Higuain mbona anakaa benchi japo alifunga magoli 30 na ni mshambuliaji bora?.


 

Leo Simba ina kibarua cha kumenyana na Biashara United kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

 

Kagere amekuwa hana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 kwenye ligi ambapo kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 ametumia dakika 47.

 

Alianza kusugua benchi mbele ya Ihefu FC wakati Simba ikishinda mabao 3-2 akitumia dakika 23 kisha mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 aliyeyusha dakika 24.


Kwa misimu miwili mfululizo Kagere amekuwa ni mfungaji bora ndani ya ligi ambapo aliibuka mfungaji bora msimu wa 2018/19 alipofunga mabao 23 kisha 2019/20 alifunga mabao 22.


Ndani ya misimu yake miwili akiwa Bongo, Kagere raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao 45 kwenye ligi pekee.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *