Posted By Posted On

MWENDO MDUNDO

NA NYEMO MALECELA, BUKOBA MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameendelea kupata raha huku wakishuhudia timu yao ikitembea mwendo mdundo baada ya jana kupata ushindi mwingine katika michuano ya Ligi Kuu Bara ikitandika Kagera Sugar bao 1-0, katika uwanja wao wa kaitaba. Bao pekee lililofungwa na kiungo Mukoko Tonombe, lilitosha kuipa timu hiyo ya Wananchi pointi
The post MWENDO MDUNDO appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA NYEMO MALECELA, BUKOBA

MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameendelea kupata raha huku wakishuhudia timu yao ikitembea mwendo mdundo baada ya jana kupata ushindi mwingine katika michuano ya Ligi Kuu Bara ikitandika Kagera Sugar bao 1-0, katika uwanja wao wa kaitaba.

Bao pekee lililofungwa na kiungo Mukoko Tonombe, lilitosha kuipa timu hiyo ya Wananchi pointi tatu ugenini na kufanikiwa kuongoza ligi hiyo ikifikisha jumla ya pointi saba.

Mukoko aliifungia Yanga dakika ya 71 akimalizia pasi ya Tuisila Kisinda aliyewalamba chenga walinzi kadhaa wa Kagera Sugar kabla ya kuweka pande hilo kwa mfungaji.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi hizo baada ya kucheza michezo mitatu, ikianza kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons kisha kuinyuka Mbeya City bao 1-0 kabla ya kupata ushindi kama huo jana dhidi ya Kagera Sugar.

Kipigo hicho kinakuwa cha pili katika michezo mitatu kwa Kagera Sugar tangu msimu huu ulipoanza, wakianza kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania, ikilazimishwa suluhu na Gwambina, kabla ya kufumuliwa na Yanga jana.

Hata hivyo, haikuwa rahisi kwa Yanga kuibuka na ushindi kwani licha ya mwenendo mbovu wa Kagera Sugar, walipata wakati mgumu kuibuka na pointi hizo tatu ugenini.

Kagera Sugar ilicheza vizuri mwanzoni mwa kipindi cha pili, lakini kukosa umakini katika eneo la ushambuliaji ndicho kilichowagharimu kupoteza mchezo huo.

Mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake ilianza kwa kasi ambapo wenyeji walitumia mipira mirefu kufika langoni mwa Yanga, huku wapinzani wao hao wakitumia mfumo wa pasi nyingi na wakati mwingine pasi ndefu kufanya mashambulizi.

Dakika ya 17, Feisal Salum alishindwa kutumia nafasi aliyoipata kuifungia Yanga bao baada ya kupokea pasi safi ya kichwa kutoka kwa Kisinda, lakini shuti lake lilishindwa kulenga lango.

Dakika 32, Michael Sarpong alipoteza nafasi ya wazi ya kuiandikia Yanga bao baada ya kupokea pande kutoka kwa Kisinda na kupiga shuti hafifu lililotua mikononi mwa mlinda mlango wa Kagera Sugar, Ramadhani Chalamanda.

Dakika ya 34, kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Mohamed Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Eric Mwijage.

Dakika ya 45, mlinzi wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi alilimwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Sarpong.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu hizo kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilianza kwa Kagera Sugar kuja na kasi mpya na kumiliki mpira zaidi kuliko Yanga.

Mabadiliko ya dakika ya 56 yaliyofanywa na kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic, ya kuwatoa Yacouba Sogne na Kibwana Shomary huku nafasi zao zikichukuliwa na Carlos Fernande ‘Carlinhos’ na Deus Kaseke yaliirudisha uhai.

Dakika ya 71, Mukoko aliindikia Yanga bao la kwanza akimalizia pande safi la Kisinda.

Dakika ya 80, mshambuliaji wa Kagera Sugar, Hassan Mwaterema, alilimwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Bakari Mwamnyeto.

Dakika ya 83, Yanga ilifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Zawadi Mauya na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.

Mbali na mchezo huo, kivumbi kingine cha ligi kilitimka katika Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa, ambapo wenyeji Tanzania Prisons iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC.

 

The post MWENDO MDUNDO appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *