Posted By Posted On

NI BALAA HESABU ZA BIASHARA UNITED BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA SIMBA

 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa hakuwa na chaguo wakati wakifungwa mabao 4-0 mbele ya Simba jana, Septemba 20 kwa kuwa walizidiwa mbinu ndani ya uwanja jambo ambalo analifanyia kazi.Biashara United ya Mara ilipoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa nje ya Mara baada ya kucheza mechi mbili za ligi na kujikusanyia pointi sita kibindoni huku ikifunga mabao mawili.Baraza amesema kuwa wamekuwa na tatizo kwenye mechi zao za ugenini jambo ambalo analifanyia kazi kwa kuwa wana mechi ngumu zinakuja mbele yao.”Hamna tatizo ndani ya timu, wachezaji wamepambana kwa ajili ya kusaka matokeo ila mwisho wa siku tumepoteza kwa kuwa tulikuwa tumezidiwa mbinu.”Ninachokifanya kwa sasa ni kutafuta mechi nyingi zaidi za kirafiki ambazo tutacheza tukiwa ugenini hizo zitatuongeza hali ya kujiamini na kufanya vema zaidi.”Kwa hiki tulichokipata kinatuumiza lakini ni matokeo ndani ya uwanja. Tunakwenda kujipanga zaidi ili kurejea kwenye kasi yetu,” amesema.Timu ya kwanza kufunga mabao zaidi ya mawili ilikuwa ni KMC iliitungua Mbeya City Uwanja wa Uhuru, kisha Simba inakuwa ya pili ndani ya ligi na ya kwanza kufunga ndani ya Uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21 kwenye ligi.,

 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa hakuwa na chaguo wakati wakifungwa mabao 4-0 mbele ya Simba jana, Septemba 20 kwa kuwa walizidiwa mbinu ndani ya uwanja jambo ambalo analifanyia kazi.


Biashara United ya Mara ilipoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa nje ya Mara baada ya kucheza mechi mbili za ligi na kujikusanyia pointi sita kibindoni huku ikifunga mabao mawili.


Baraza amesema kuwa wamekuwa na tatizo kwenye mechi zao za ugenini jambo ambalo analifanyia kazi kwa kuwa wana mechi ngumu zinakuja mbele yao.


“Hamna tatizo ndani ya timu, wachezaji wamepambana kwa ajili ya kusaka matokeo ila mwisho wa siku tumepoteza kwa kuwa tulikuwa tumezidiwa mbinu.


“Ninachokifanya kwa sasa ni kutafuta mechi nyingi zaidi za kirafiki ambazo tutacheza tukiwa ugenini hizo zitatuongeza hali ya kujiamini na kufanya vema zaidi.


“Kwa hiki tulichokipata kinatuumiza lakini ni matokeo ndani ya uwanja. Tunakwenda kujipanga zaidi ili kurejea kwenye kasi yetu,” amesema.


Timu ya kwanza kufunga mabao zaidi ya mawili ilikuwa ni KMC iliitungua Mbeya City Uwanja wa Uhuru, kisha Simba inakuwa ya pili ndani ya ligi na ya kwanza kufunga ndani ya Uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21 kwenye ligi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *