Posted By Posted On

SABABU YA MUANGOLA WA YANGA KUANZIA BENCHI HII HAPA

 KOCHA Mkuu wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema kuwa kiungo wake raia wa Angola, Carlos Fernandes ‘Carlinhos ana nafasi ya kuja kufanya vizuri kwenye mechi zijazo ikiwa akiwa fiti asilimia 100.Carlinhos amekuwa gumzo ndani ya Yanga ambapo kwenye mechi mbili ameshindwa kuyeyusha dakika zote 90 zaidi ya kuanzia benchi.Kibindoni ana pasi moja ya bao ambayo alimpa beki kisiki wa Yanga, Lamine Moro wakati timu yake ikishinda mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0, Uwanja wa Mkapa.Krmpotic amesema:”Bado hajawa fiti kwa asilimia 100 ndio maana sijampa muda wa kuwa ndani ya kikosi cha kwanza kwenye mechi za hivi karibuni.”Sababu kubwa ni kwamba hajacheza kwa muda mrefu wakati akiwa Angola hivyo lazima niendel naye taratibu kumuweka sawa na akizoea mazingira basi atakuwa imara zaidi ya sasa,” amesema.Yanga kwa sasa ipo Dar inajipanga kwa ajili ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. ,


 KOCHA Mkuu wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema kuwa kiungo wake raia wa Angola, Carlos Fernandes ‘Carlinhos ana nafasi ya kuja kufanya vizuri kwenye mechi zijazo ikiwa akiwa fiti asilimia 100.


Carlinhos amekuwa gumzo ndani ya Yanga ambapo kwenye mechi mbili ameshindwa kuyeyusha dakika zote 90 zaidi ya kuanzia benchi.


Kibindoni ana pasi moja ya bao ambayo alimpa beki kisiki wa Yanga, Lamine Moro wakati timu yake ikishinda mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0, Uwanja wa Mkapa.

Krmpotic amesema:”Bado hajawa fiti kwa asilimia 100 ndio maana sijampa muda wa kuwa ndani ya kikosi cha kwanza kwenye mechi za hivi karibuni.


“Sababu kubwa ni kwamba hajacheza kwa muda mrefu wakati akiwa Angola hivyo lazima niendel naye taratibu kumuweka sawa na akizoea mazingira basi atakuwa imara zaidi ya sasa,” amesema.


Yanga kwa sasa ipo Dar inajipanga kwa ajili ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *