Posted By Posted On

SIMBA YAIPIGA 4G BIASHARA UNITED KWA MKAPA

 KIKOSI cha Simba leo kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.Kasi ya Simba leo Septemba 20, Uwanja wa Mkapa ilianza ndani ya dakika 10 za mwanzo ambapo ilipata bao la kwanza dakika ya 9 na la pili dakika ya 26 kupitia kwa Clatous Chama aliyetumia pasi za kiungo mwenzake Luis Miqussone,’Konde Boy’.Bao la tatu kwa Simba lilipachikwa na mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi hicho Meddie Kagere dakika ya 52 kwa pasi ya Konde Boy.Chris Mugalu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi alipachika bao la nne na la mwisho kupitia kwa pasi ya Chama ilikuwa dakika 84.Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi saba kibindoni ikiwa nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Azam FC ambao wameshinda leo bao 1-0 mbele ya Mbeya City mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.Huu ni mchezo wa kwanza kwa Biashara United kupoteza ndani ya msimu wa 2020/21 wakiwa ugenini.Licha ya kupoteza kipa namba moja wa Biashara United alitimiza majukumu yake ambapo aliokoa moja ya hatari matata ndani ya lango lake iliyopigwa na Luis.,


 KIKOSI cha Simba leo kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kasi ya Simba leo Septemba 20, Uwanja wa Mkapa ilianza ndani ya dakika 10 za mwanzo ambapo ilipata bao la kwanza dakika ya 9 na la pili dakika ya 26 kupitia kwa Clatous Chama aliyetumia pasi za kiungo mwenzake Luis Miqussone,’Konde Boy’.


Bao la tatu kwa Simba lilipachikwa na mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi hicho Meddie Kagere dakika ya 52 kwa pasi ya Konde Boy.

Chris Mugalu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi alipachika bao la nne na la mwisho kupitia kwa pasi ya Chama ilikuwa dakika 84.


Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi saba kibindoni ikiwa nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Azam FC ambao wameshinda leo bao 1-0 mbele ya Mbeya City mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Huu ni mchezo wa kwanza kwa Biashara United kupoteza ndani ya msimu wa 2020/21 wakiwa ugenini.


Licha ya kupoteza kipa namba moja wa Biashara United alitimiza majukumu yake ambapo aliokoa moja ya hatari matata ndani ya lango lake iliyopigwa na Luis.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *