Posted By Posted On

YANGA WAREJEA DAR, HESABU ZAO ZIPO KWENYE KOMBE TU

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu kubwa ndani ya Ligi Kuu Bara ni kuweza kutwaa ubingwa ambao waliokusa kwa misimu mitatu mfululizo jambo ambalo linawafanya wapambane kusaka pointi tatu kwenye kila mchezo.Leo kikosi kimerejea Dar baada ya kuibukia Kagera ambapo kilikuwa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 19 na kilishinda kwa bao 1-0.Bao pekee la ushindi lilifungwa na Tonombe Mukoko dakika ya 72 baada ya mabeki wa Kagera Sugar kushindwa kuokoa hatari iliyopigwa na Tuisila Kisinda.Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotick amesema kuwa bado wanahitaji muda wa kuendelea kuwa bora kwa kuwa kuna mechi nyingi za kucheza.”Wachezaji wanatimiza majukumu yao vizuri ila bado tuna mechi nyingine mbele ambazo ni muhimu kwetu kushinda ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.Yanga ina kibarua kingine Septemba 27 itakuwa mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. ,


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu kubwa ndani ya Ligi Kuu Bara ni kuweza kutwaa ubingwa ambao waliokusa kwa misimu mitatu mfululizo jambo ambalo linawafanya wapambane kusaka pointi tatu kwenye kila mchezo.


Leo kikosi kimerejea Dar baada ya kuibukia Kagera ambapo kilikuwa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 19 na kilishinda kwa bao 1-0.Bao pekee la ushindi lilifungwa na Tonombe Mukoko dakika ya 72 baada ya mabeki wa Kagera Sugar kushindwa kuokoa hatari iliyopigwa na Tuisila Kisinda.


Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotick amesema kuwa bado wanahitaji muda wa kuendelea kuwa bora kwa kuwa kuna mechi nyingi za kucheza.


“Wachezaji wanatimiza majukumu yao vizuri ila bado tuna mechi nyingine mbele ambazo ni muhimu kwetu kushinda ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.


Yanga ina kibarua kingine Septemba 27 itakuwa mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *