ALICHOSEMA KOCHA MKUU YANGA BAADA MECHI DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga imeifunga Kagera Sugar bao 1-0 na kupanda kileleni kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kufikisha pointi saba.

Mukoko Tonombe ndiye aliyepeleka kilio Kagera Sugar baada ya kufunga bao dakika ya 71 akimalizia pasi ya Tuisila Kisinda.
Baada ya kufunga bao hilo Mukoko alikimbia hadi kwenye kibendera cha kona na kuwaita wenzake na kuwaambia wakae chini kisha kuonekana kama anawafundisha hivi hivyo kuamsha shangwe kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo kwenye uwanja wa Kaitaba ambao muda mwingi walikuwa kimya.
Hata hivyo Yanga licha ya kushinda mchezo huo na kumiliki mpira lakini ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi za kupata bao jambo ambalo hata kocha wa kikosi hicho,Zlatko Krmpotic  amekiri.
Zlatko amewapa hongera wachezaji wake kwa ushindi licha ya kukiri mchezo ulikuwa mgumu kwani Kagera Sugar ni timu nzuri.
“Tulitengeneza nafasi mbili tatu na kuweza kutumia moja hivyo nawapa hongera timu yangu kwa ushindi ingawa nahitaji kuona tukicheza vizuri zaidi katika michezo ijayo”, amesema Zlatko.

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *