Posted By Posted On

HESABU ZA YANGA ZIPO NAMNA HII KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA MTIBWA

 LAMINE MORO, beki kisiki wa Yanga, amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zao zote ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.Kwa sasa Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Beki huyo amesema; “Kikubwa tunahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki ili tuweze kuendelea kuwa bora kwani sapoti yao ni muhimu kwetu katika mchezo yoyote. ”Tuna waheshimu sana Mtibwa kutokana na ubora ambao walionyesha katika mechi zao lakini sisi tutaingia uwanjani kucheza kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” amesema Lamine. Kikosi cha Yanga kimerejea Dar es Salaam baada ya kushinda mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 19 bao 1-0,  bao pekee la ushindi lililofungwa na Tonombe Mukoko dakika ya 72 baada ya mabeki wa Kagera Sugar kushindwa kuokoa hatari iliyopigwa na Tuisila Kisinda. Yanga ipo nafasi ya tatu nyumba ya vinara Azam wenye alama 9, huku watani zao Wekundu wa Msimbazi Simba wakiwa nafasi ya pili  kwa alama 7.,

 


LAMINE MORO, beki kisiki wa Yanga, amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zao zote ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Kwa sasa Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

Beki huyo amesema; “Kikubwa tunahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki ili tuweze kuendelea kuwa bora kwani sapoti yao ni muhimu kwetu katika mchezo yoyote.

 

”Tuna waheshimu sana Mtibwa kutokana na ubora ambao walionyesha katika mechi zao lakini sisi tutaingia uwanjani kucheza kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” amesema Lamine.

 

Kikosi cha Yanga kimerejea Dar es Salaam baada ya kushinda mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 19 bao 1-0,  bao pekee la ushindi lililofungwa na Tonombe Mukoko dakika ya 72 baada ya mabeki wa Kagera Sugar kushindwa kuokoa hatari iliyopigwa na Tuisila Kisinda.

 

Yanga ipo nafasi ya tatu nyumba ya vinara Azam wenye alama 9, huku watani zao Wekundu wa Msimbazi Simba wakiwa nafasi ya pili  kwa alama 7.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *