Posted By Posted On

KAGERA SUGAR MAJANGA MATUPU, DAKIKA 270 BILA POINTI KIBINDONI

 KLABU ya Kagera Sugar imeaanza kwa majanga msimu wa 2020/21 baada ya safu yake ya ushambuliaji kushindwa kufunga kwenye mechi zake tatu mfululizo ambazo ni dakika 270.Safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na Mbaraka Yusuph ambaye ni ingizo jipya kutoka Azam FC pamoja na Mohamed Ibrahim,’Mo Ibra’ aliyeibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Namungo.Safu yao ya ulinzi inayoongozwa na Ally Mtoni,’Sonso’ imeruhusu makipa wake kuokota mabao mawili nyavuni kwenye mechi mbili kati ya tatu ambazo wamecheza.Ilianza kutunguliwa na JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba kupitia kwa Adam Adam kisha ililazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC, Uwanja wa Gwambina kisha juzi ilikubali kufungwa bao 1-0 ikiwa Kaitaba mbele ya Yanga.Ndani ya dakika 270, Kagera Sugar haijaambulia pointi mpaka sasa ikiwa imecheza mechi mbili na haijafunga hata bao jambo linalompasua kichwa Kocha Mkuu Mecky Maxime ambaye amesema kuwa anayafanyia kazi makosa yao.Kwenye mechi tatu wakati ikisaka pointi sita haijaambulia hata pointi kibindoni huku ikiwa imepoteza mechi zake zote mbili za mwanzo Uwanja wa Kaitaba.,


 KLABU ya Kagera Sugar imeaanza kwa majanga msimu wa 2020/21 baada ya safu yake ya ushambuliaji kushindwa kufunga kwenye mechi zake tatu mfululizo ambazo ni dakika 270.

Safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na Mbaraka Yusuph ambaye ni ingizo jipya kutoka Azam FC pamoja na Mohamed Ibrahim,’Mo Ibra’ aliyeibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Namungo.

Safu yao ya ulinzi inayoongozwa na Ally Mtoni,’Sonso’ imeruhusu makipa wake kuokota mabao mawili nyavuni kwenye mechi mbili kati ya tatu ambazo wamecheza.

Ilianza kutunguliwa na JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba kupitia kwa Adam Adam kisha ililazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC, Uwanja wa Gwambina kisha juzi ilikubali kufungwa bao 1-0 ikiwa Kaitaba mbele ya Yanga.

Ndani ya dakika 270, Kagera Sugar haijaambulia pointi mpaka sasa ikiwa imecheza mechi mbili na haijafunga hata bao jambo linalompasua kichwa Kocha Mkuu Mecky Maxime ambaye amesema kuwa anayafanyia kazi makosa yao.


Kwenye mechi tatu wakati ikisaka pointi sita haijaambulia hata pointi kibindoni huku ikiwa imepoteza mechi zake zote mbili za mwanzo Uwanja wa Kaitaba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *