Posted By Posted On

KMC KAMILI GADO KUIVAA MWADUI FC LEO

OFISA Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Septemba 21 dhidi ya Mwadui FC.KMC imeanza kwa kasi msimu mpya wa 2020/21 ambapo kwenye mechi mbili za mwanzo ilishinda kwa zote na kusepa na pointi tatu mazima na iliweza kuongoza ligi kwenye mzunguko wa pili na kwa kwanza ilipofikisha pointi sita kibindoni. Christina amesema kuwa kikosi kipo tayari kuendeleza rekodi za kushinda mechi zake kwa kuwa kila kitu kipo sawa kuanzia wachezaji na benchi la ufundi.”Kikosi kipo sawa na tunahitaji ushindi ili kuendelea na kasi yetu ambayo tumeianza, tunahitaji kuongoza ligi ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji na kurejesha morali zaidi kila wakati,” amesema.Mechi mbili ambazo Mwadui FC imecheza kwa msimu wa 2020/21 haijashinda hata moja hivyo leo itacheza kwa tahadhari kubwa kusaka pointi tatu muhimu jambo litakaloongeza ushindani.,

OFISA Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Septemba 21 dhidi ya Mwadui FC.

KMC imeanza kwa kasi msimu mpya wa 2020/21 ambapo kwenye mechi mbili za mwanzo ilishinda kwa zote na kusepa na pointi tatu mazima na iliweza kuongoza ligi kwenye mzunguko wa pili na kwa kwanza ilipofikisha pointi sita kibindoni.


 Christina amesema kuwa kikosi kipo tayari kuendeleza rekodi za kushinda mechi zake kwa kuwa kila kitu kipo sawa kuanzia wachezaji na benchi la ufundi.


“Kikosi kipo sawa na tunahitaji ushindi ili kuendelea na kasi yetu ambayo tumeianza, tunahitaji kuongoza ligi ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji na kurejesha morali zaidi kila wakati,” amesema.

Mechi mbili ambazo Mwadui FC imecheza kwa msimu wa 2020/21 haijashinda hata moja hivyo leo itacheza kwa tahadhari kubwa kusaka pointi tatu muhimu jambo litakaloongeza ushindani.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *