Posted By Posted On

KOCHA MKUU ASAKA KIKOSI CHA KWANZA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Zlatko Krmpotic, amekuwa akitumia wachezaji tofauti katika kikosi chake cha kwanza katika michezo yote mitatu iliyochezwa nyumbani na ugenini.

Mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons alianza na kundi kubwa la wachezaji wazawa na wageni wawili tu, ambapo kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri hadi alipofanya mabadiliko.

Mchezo uliofuata alianzisha wachezaji wengi waliocheza kipindi cha pili katika mchezo dhidi ya Prisons na kufanikiwa kuvuna pointi tatu dhidi ya Mbeya City ndani ya Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons.

Lakini sasa kocha huyo amepanga kutumia mechi tano zijazo kusaka kikosi cha kwanza, ambacho hakitakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kama ilivyotokea kwenye michezo iliyopita ya ligi hiyo.

Hatua hiyo,  itaibuka vita kwa wachezaji wake kwani kila mmoja atalazimika kuonesha juhudi mazoezini ili kupenya kikosini.

Katika kufanikisha hilo, tayari Yanga imecheza michezo mitatu ya Ligi Kuu na miwili tu,  imesalia kabla uamuzi mgumu haujatolewa na kocha huyo raia wa Serbia.

Wakati huo huo, kikosi cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi kikitokea mkoani Kagera na wachezaji kupewa mapumziko ya siku moja kabla ya kuanza maandalizi ya kuwakabiji Mtibwa Sugar.

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *