Posted By Posted On

MCHEZO MZIMA WA SIMBA KUMALIZANA NA BIASHARA UNITED KWA 4G ULIKUWA HIVI

 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jana Septemba 20 waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.Mchezo huo Simba ilianza kwa kasi ndani ya dakika 10 za mwanzo na ilipachika bao la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa kiungo Clatous Chama aliyepachika na bao la pili pia dakika ya 26 kwa pasi za Luis Miqussone.Mabao mengine yalipachikwa na Meddie Kagere ambaye alifunga bao lake la kwanza kwa msimu wa 2020/21 dakika ya 52 kwa pasi ya Luis huku lile la nne likipachikwa na Chris Mugalu dakika 85 ambaye alimalizia pasi ya Chama aliyekuwa nyota wa mchezo kwa jana.Kasi ya Simba Uwanja wa Mkapa iliwapa shida wapinzani wao Biashara United ambao kwa mara ya kwanza ndani ya ligi wanapoteza baada ya kucheza mechi mbili za awali bila kupoteza walipokuwa Uwanja wa Karume. Larry Bwalya wa Simba alianza vurugu sekunde ya 50 ya mchezo kwa kusepa na kijiji chake kabla ya kupiga shuti lililokwenda nje kidogo ya lango.Meddie Kagere dakika ya 14 alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 baada ya kupiga kichwa kilichookolewa na mlinda mlango Daniel Mgore ambaye alionyesha uimara licha ya kufungwa.Dakika ya 44, Bwalya pia alipiga shuti lililopaa juu baada ya Simba kugongeana pasi fupifupi.Kiungo wa Brazil, Gerson Fraga alianza mchezo wake wa kwanza kwa kushindwa kumaliza dakika 90 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Said Ndemla dakika ya 8.Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi saba kibindoni ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu na kibindoni imefunga mabao saba nafasi ya pili kinara akiwa ni Azam FC mwenye pointi 9. Kikosi cha Simba kilichoanzaAishi Manula,Shomari Kapombe,Mohammed Hussein,Joash Onyango,Pascal Wawa,Gerson Fraga, Luis Miquissone,Mzamiru Yassin,Meddie Kagere, Larry Bwalya, Clatous Chama. Kikosi cha Biashara United kilichoanzaDaniel Mgore ,Ally Kombo ,Ramadhan Chombo ,Deogratius Judika,Tariq Abdallah,Kelvin Friday,Mpapi Salum, Mustha Khamis, Lenny Vedastus, Abdulmajid Mangaro,Omary Nassoro .,

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jana Septemba 20 waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo Simba ilianza kwa kasi ndani ya dakika 10 za mwanzo na ilipachika bao la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa kiungo Clatous Chama aliyepachika na bao la pili pia dakika ya 26 kwa pasi za Luis Miqussone.

Mabao mengine yalipachikwa na Meddie Kagere ambaye alifunga bao lake la kwanza kwa msimu wa 2020/21 dakika ya 52 kwa pasi ya Luis huku lile la nne likipachikwa na Chris Mugalu dakika 85 ambaye alimalizia pasi ya Chama aliyekuwa nyota wa mchezo kwa jana.

Kasi ya Simba Uwanja wa Mkapa iliwapa shida wapinzani wao Biashara United ambao kwa mara ya kwanza ndani ya ligi wanapoteza baada ya kucheza mechi mbili za awali bila kupoteza walipokuwa Uwanja wa Karume.

 Larry Bwalya wa Simba alianza vurugu sekunde ya 50 ya mchezo kwa kusepa na kijiji chake kabla ya kupiga shuti lililokwenda nje kidogo ya lango.

Meddie Kagere dakika ya 14 alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 baada ya kupiga kichwa kilichookolewa na mlinda mlango Daniel Mgore ambaye alionyesha uimara licha ya kufungwa.

Dakika ya 44, Bwalya pia alipiga shuti lililopaa juu baada ya Simba kugongeana pasi fupifupi.

Kiungo wa Brazil, Gerson Fraga alianza mchezo wake wa kwanza kwa kushindwa kumaliza dakika 90 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Said Ndemla dakika ya 8.


Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi saba kibindoni ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu na kibindoni imefunga mabao saba nafasi ya pili kinara akiwa ni Azam FC mwenye pointi 9.

 

Kikosi cha Simba kilichoanza
Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohammed Hussein,Joash Onyango,Pascal Wawa,Gerson Fraga, Luis Miquissone,Mzamiru Yassin,Meddie Kagere, Larry Bwalya, Clatous Chama.

 

Kikosi cha Biashara United kilichoanza

Daniel Mgore ,Ally Kombo ,Ramadhan Chombo ,Deogratius Judika,
Tariq Abdallah,Kelvin Friday,Mpapi Salum, Mustha Khamis, Lenny Vedastus, Abdulmajid Mangaro,Omary Nassoro .

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *