MFUMO BADO TATIZO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mkuu Yanga Krmpotic alisema kuwa bado kuna changamoto mbalimbali wanaendelea kuzifanyia kazi katika kikosi mbali na kufurahia ushindi lakini bado kikosi chake hakijacheza na kumfurahisha.

Krmpotic alisema hafurahii kila kitu ingawa timu yake inashinda na kutokana na upya wa wachezaji wake wataendelea kujiimarisha taratibu katika mechi zao ingawa pia amekubali ushindani kutoka kwa timu pinzani.

“Siwezi kuridhika na kila kitu, lakini nafurahi kuona timu inashinda, kwasasa kucheza nyumbani hata ugenini sio rahisi, lakini narudia hapa, bado tunatengeneza timu mambo mazuri hayawezi kuja kwa haraka sana,” alisema Krmpotic, ambaye ameshafurahia ushindi mara mbili katika mechi tatu.

“Kuna wakati tunatakiwa tutumie zaidi nafasi ambazo tunatengeneza katika mechi, angalia jana (juzi) kuna nafasi ya uhakika Carlinhos (Carlos Fernandez) aliipoteza, hili si jambo zuri, lakini bado kuna kazi tunatakiwa kuifanya.

Licha ya kushinda juzi na kupata pointi tatu, wachambuzi wa soka nchini walidai bado Yanga ina mambo mengi ya kuyaboresha, ingawa kubwa ni mfumo.

Mchezaji wa zamani wa timu hiyo na mchambuzi wa soka, Ally Mayay alisema mabingwa hao wa zamani wanapata matokeo kwa uwezo wa wachezaji, lakini si kwa mfumo.

“Timu inatumia ‘basics’ za ulinzi, ‘attaking’, inapata matokeo kwa uwezo wa mchezaji mmoja-mmoja,” alisema.

Mayay alisema kwenye mchezo na Kagera, kama Yanga wangekutana na timu yenye mpango wa kueleweka, Kagera wangepata urahisi wa kuzuia na kuleta madhara kwa Yanga.

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *