Posted By Posted On

MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.Yanga itamenyana na Mtibwa Sugar ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao uliochezwa Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo nayo imetoka kushinda mbele ya Ihefu FC kwa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine, Septemba 18.Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa wapo tayari kumenyana na Yanga wanahitaji kupata pointi tatu muhimu.“Ushindi ndio kitu ambacho tunakihitaji hakuna jambo jingine. Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini wasitarajie kupata wepesi kwetu tutapambana kushinda,” alisema Kifaru.,


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Yanga itamenyana na Mtibwa Sugar ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao uliochezwa Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.

Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo nayo imetoka kushinda mbele ya Ihefu FC kwa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine, Septemba 18.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa wapo tayari kumenyana na Yanga wanahitaji kupata pointi tatu muhimu.

“Ushindi ndio kitu ambacho tunakihitaji hakuna jambo jingine. Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini wasitarajie kupata wepesi kwetu tutapambana kushinda,” alisema Kifaru.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *