Posted By Posted On

MWAMNYETO ATOLEA UFAFANUZI, TUHUMA KUSHIKA MPIRA MECHI DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Beki Bakar Mwamnyeto amesema amesikia kelele za baadhi ya wadau wakisema alishika mpira, mechi dhidi Kagera Sugar.

Tukio la dakika ya 46 ya nyongeza kipindi cha kwanza krosi ya mshambuliaji Vitalis Mayanga ilionekana kama imemgonga Mwamnyeto katika mkono wake wa kulia na tukio hilo lilitafsiriwa ameushika na mwamuzi kukausha.

Hata hivyo, akizungumza jana, Mwamnyeto alisema ameona mijadala hiyo kupitia mitandao ya kijamii, ila sio kweli kama mpira ulimgonga katika mkono wake na wala hakukaribia.

“Mpira hakufika kabisa mkononi, nimeona hilo watu wanasema lakini ukweli ni kwamba mpira haukunifikia kabisa katika eneo la mkono hao wanaosema kazi kwao,” alisema Mwamnyeto.

Beki huyo ghali nchini alisema kwa wachezaji wazawa alisema alikuwa makini katika shambuliao na namna ile na alitangulia kuuficha mikono yake nyuma, ingawa baadaye aliachia baada ya kuona mpira haukaribii mikono yake.

“Watu watulie wanapoliangalia lile tukio unajua kwanza nilianza kuweka mikono nyuma, lakini nilipoona mpira hauwezi kunifikia mikononi nikaiachia na ukanigonga kifuani pembeni kidogo.”

Alisema kwa nafasi ambayo mwamuzi wa kati alikuwa amesimama isingekuwa tabu kwake kuliona tukio hilo na wala halimchanganyi na ana uhakika hakuunawa.

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *